Prof.Riziki Shemdoe amekagua ujenzi wa shule shikizi ya msingi ya  Mwera pamoja ujenzi wa shule  mpya ya bweni ya sekondari Kimang'a zilizopo wilayani Pangani Mkoani Tanga.


Prof. Shemdoe amefanya ukaguzi huo wakati wa ziara yake Wilayani humo mapema tarehe 16.11.2021z


Akikagua shule hizo Prof. Shemdoe ameonyeshwa kuridhishwa na hatua ya ujenzi wa Shule hizo hasa shule mpya ya sekondari ya bweni ya Kimang'a ambapo amefurahishwa na muda mchache waliotumia katika ujenzi huo  huku akiwataka viongozi wa wilaya hiyo kufanya kazi kwa juhudi ili kuhakikisha shule hizo zinakamilika kabla ya  disemba 15, 2021 kwa ajili ya wanafunzi kuanza masomo ifikapo Januari,2021.


"Nitoe msisitizo madarasa haya  ifikapo tarehe 15 disemba 2021 vile vyumba vya madarasa viwe vimekamilika, tukabidhiwe ili kujiandaa sasa kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi Januari". Prof.Riziki Shemdoe katibu mkuu TAMISEMI


Pia prof Mdoe amewataka kuangalia namna ya kubadilisha  aina ya ujenzi kwa kutumia mapaa mawili badala ya manne  ili kupunguza gharama za ujenzi.

Share To:

Post A Comment: