Na Asila Twaha, Morogoro


TAMISEMI Queens mambo  safi wajizolea magoli 40 na alama 2 mchezo wa pete baada ya timu pinzani ya Ujenzi kushindwa kufika uwanjani.


Mchezo huo ulipangwa kuchezwa Oktoba 25, 2021 majira ya saa 8 mchana katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro lakini mpaka muda wa mchezo unafika timu ya Ujenzi ilikua haijawasili uwanjani hapo na mwamuzi wa mchezo kuamru alama ziende kwa TAMISEMI Queens.


Huo ulikuwa ni mchezo wao wa nne kucheza katika mashindano ya SHIMIWI  yanayoendelea  wakiwa wameshinda michezo yote.


TAMISEMI Queens wametinga hatua ya 16 bora katika mashindano  hayo  wakiwa hawajapoteza mchezo wowote katika mechi walizocheza.


Baada ya kutoonekana uwanjani timu ya Ujenzi kocha wa timu hiyo Mwamvita Mzee amesema timu yake haijaweza kufika uwanjani kutokana na kuwa na majeruhi wengi na kuwaomba radhi timu ya TAMISEMI.


Kwa upande wa kocha wa TAMISEMI Queens Maimuna Kitete ameeleza siri ya mafaniko ya timu yake kuwa ni wachezaji kujituma, ushirikiano wa viongozi na nidhamu mchezoni na kuahidi mashabiki wa timu yake kufanya vizuri zaidi katika michezo inayofuata.


Kwa mujibu wa sheria ya mchezo wa pete timu isipofika uwanjani wapinzani wake hupewa magoli 40 na alama 2.

Share To:

Post A Comment: