NA  HERI SHABAN


KAMPUNI ya WAHENGA ALUMINIUM inatarajia kujenga vyoo vya Shule ya sekondari ya Kisungu Kinyelezi wilaya Ilala.


Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Wahenga Aluminium Tanzania John Ryoba Mrema wakati wa Mahafali ya 12 shule ya sekondari ya Kisungu Wilaya ya Ilala


"Miundombinu ya Shule ya Sekondari ya Kisungu nichakavu nimejionea nitaboresha sambamba na ujenzi wa vyoo vya shule ambavyo matundu yake hayatoshelezi "alisema Ryoba


John Ryoba alisema amefanya ziara katika shule hiyo na kuanza mchakato kutatua baadhi ya changamoto za shule ikiwemo kuchonga barabara nayo ilitekelezwa na kufanya mazingira ya kusoma si rafiki.


Alisema anaunga mkono serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sekta ya elimu akiwa mdau wa elimu kumsaidia Rais Samia Hassan Suluhu mpango wa elimu bila malipo.


Alisema Taifa lolote ili liweze kuendelea lazima uwajengee misingi imara wanafunzi katika sekta ya elimu ili kuja kuibua wana Sayansi ,madaktari na Mawaziri wa baadae .


Ametoa wito kwa Serikali katika shule za kata kuwekeza walimu wengi wa sayansi na Mahabara za vitendo ili watoto wetu waweze kupata elimu bora


Wakati huohuo John Ryoba alisema Mwanafunzi wa kwanza katika shule hiyo atamsomesha shule mpaka kulipa ada ya elimu yake.


Mkuu wa shule ya sekondari ya Kisungu Arnold Tenganamba alisema  shule ya Sekondari ya Kisungu mwaka 2007  kwa sasa madarasa kumi mabovu haina Jengo la utawala.


Mwalimu Tenganamba alisema kitaaluma shule hiyo inafanya vizuri kila mwaka ufaulu unaongezeka  mwaka 2016 ufaulu asilimia 54 mwaka 2017 ufaulu asilimia 36 mwaka 2018 ufaulu asilimia 64 mwaka 2019 ufaulu asilimia 60 mwaka 2020 ufaulu asilimia 65.


Akizungumzia changamoto Walimu wa Sayansi,Biology.Chemistry na Hesabu


Share To:

Post A Comment: