Monday, 4 October 2021

ENDELEENI NA UTARATIBU WA KUFANYA MAZOEZI MARA KWA MARA-ULEGA

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na washiriki wa mbio za  Jogging kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo na mkoa wa Dar es Salaam baada ya kumaliza kushiriki Joggingl leo kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Vikindu wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.Mhe Ulega amewaomba washiriki wa mbio hizo kufanya mazoezi kwa ajili ya afya pia amewapongeza waliojitokeza kushiriki wa mazoezi hayo huku akiwasisitiza kuendeleza utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara ilikuweka mwili sawa.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega (katikati) leo ameshiriki mbio za pole pole Jogging na vijana wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya  Mkuranga na mkoa wa Dar es Salaam.kushoto ni Diwani wa kata ya Vikindu Mohammed Maundu. (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega (wa kwanza kuli)  akishiriki mazowezi baada ya kumaliza kukimbia mbio za pole pole Jogging na vijana wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya  Mkuranga na mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Vikindu wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani

Mazowezi yakiendelea.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na vikundu  vya 
Jogging mara maada ya kumaliza kushiriki mazowezi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Vikindu wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment