Na Rhoda Simba, Dodoma



ZAIDI ya asasi za kiraia 150 zinatarajiwa kushiriki katika wiki ya AZAKI lengo ikiwa ni kuona Mchango wa AZAKI  kwa Maendeleo ya Taifa ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Job Ndugai.


Akiongea leo October 22  na waandishi wa habari jijini hapa Nesia Mahenge Mkurugenzi Mkazi CBM Tanzania,amesema wiki ya AZAKI itafanyika kuanzia Oktoba 23 hadi 28 oktoba 2021 ambapo  wiki hiyo itaambatana na maonesho mbalimbali ya kazi za AZAKI katika ukumbi wa  Jakaya kikwete.


 "Kesho ni siku maalum na ni mwanzo wa siku ya AZAKI ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali zitakazoeleza mchango mkubwa watakaoenda kuufanya kwa mendeleo ya nchi yetu," Amesema  Mahenge


Na kuongeza kusema "katika siku ya kwanza ya wiki ya AZAKI kuanzia saa1 asubuhi kutakuwa na matembezi kuanzia Shule ya Dodoma sekondari hadi ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete ambapo ndio tutaenda kufanya ufunguzi wa wiki hiyo," Amesema Mahenge


Pia amesema katika wiki hiyo kutakuwa na wageni mbalimbali kutoka mashirika ya ndani na nje ya nchi ambapo kwa upande wa viongozi wa kitaifa watakuwepo Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony  Mtaka,Mstahiki Meya Devis Mwamfupe ,Mkuu wa Wilaya Jabiri Shekimweri,Msajili wa NGos na Mabalozi toka nchi mbalimbali Canada,sizaland,ubalozi wa Denmark kwa hapa nchini Tanzania.


"Pia kutakuwa na banda maalum kwaajili ya utoaji wa chanjo ya uviko  19 ambapo watu wenye uhitaji watachanja kwa hiari yao wenyewe na kuanzia tarehe 25 hadi 28  kutakuwa na majadiliano royal village tarehe 23 na24 ," Amesema  Mahenge


Kwa upande wake Reynald  Maeda Mkurugenzi Mtendaji UNA Tanzania akizungumzia AZAKI kwa ujumla amesema  AZAKI imeleta maendeleo katika sekta ya afya katika kuleta huduma ya afya karibu na wananchi masuala ya ujenzi wa vituo vya afya,kusomesha madaktari pamoja na vifaa,wamekuwa wakifuata miongozo mbalimbali ya Serikali kama wabia wanataka kufanya utafiti kupata picha kamili ili kuweza kuona mchango wa AZAKI kwa nchi ya Tanzania.


" Katika wiki hii Mashirika zaidi ya 150 yamejitokeza kushiriki katika wiki ya AZAKI  ni kweli usiopingika michango ya AZAKI imekuwa Zaidi kama nchi pia Serikali imefanya juhudi katika kusaidia maendeleo ya nchi,kupitia wiki ya AZAKI ambayo ya kwanza yalianza 2018 kuangalia wanatoka wapi na kaungalia namna wanakuwa na michango ya nchi endelevu na kuhakikisha shughuli zao zinawafikia wananchi ili kuweka mikakati ya kujipima katika miaka ijayo na kuongeza nguvu" amesema Maeda


Aidha amesema matukio mengine ni utoaji wa tuzo kwa asasi za kiraia kutambua mchango wao katika maeneo wanayofanya kazi na mgeni rasmi atakuwa Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dorothi Gwajima na watafunga wiki ya AZAKI siku ya alhamis  tarehe 28.


Hata hivyo maonesho hayo yataambatana na burudani mbalimbali  kutoka wanamuziki wa kizazi kipya huku yakibebwa na kauli mbiu isemayo AZAKI kwa maendeleo. 

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: