Mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa.

KUTOKANA na uwepo wa vivutio vingi vya utalii mkoani Iringa,Mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amesema mkoa huo unavyo vivutio vingi vya utalii na kutoa wito kwa watalii kujitokeza kwa wingi ili kujionea maajabu.

Alitoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari wanawake takribani 30 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini walipomtembelea ofisini kwake ambapo alisema utalii unachangia kukuza pato la mkoa wa Iringa.

‘’Mpaka sasa tayari utalii unachangia kwa kiasi kikubwa pato la mkoa wetu kwa sababu wapo watalii wengi ambao wanakuja,wapo watalii wengi ambao wanataka kujifunza kuhusu chief mkwawa,kwenda Ruaha pamoja na makumbusho ambayo yanaelezea kuhusua mkoa wa Iringa’’alisema Ngwada.

Meya Ngwanda amesema mkoa wa Iringa ni pahala pazuri kwa ajili ya kuwekeza kwa sababu ni jirani na makao makuu ya nchi.

‘’Bado tunahitaji watu wengi waje wawekezi Iringa,halmashauri yetu ya manispaa ndio sehemu sahihi kwa sababu kuna maeneo ya kuwekeza kwa ajili ya hotel,majengo makubwa kwa sababu ni kweli mtu anaposhindwa kufamya jambo katika mkoa wa Dodoma kama akitaka sehemu ya karibu kufanya jambo lake basi mkoa wa Iringa ni sehemu ya karibu zaidi ambayo kwa kweli tunachukua nafasi hii kuwakaribisheni watu wote’’amesema Meya Ngwanda.
Share To:

Post A Comment: