Sunday, 26 September 2021

HOSPITALI YA HARMONY KUJENGA CHUO CHA MANESI BONYOKWA

 


NA HERI SHAABAN


HOSPITALI ya Harmony Memorial Polyclinic kufungua chuo cha Manesi  Kata ya Bonyokwa Wilayani Ilala Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Hospitali ya kisasa  Harmony Memorial Polyclinic Julian Mmari wakati wa uzinduzi wa Hospitali hiyo iliyozinduliwa na Mbunge wa Segerea   Bonah Ladslaus Kamoli.


Mkurugenzi Mmari alisema mikakati ya Hospitali ya Harmony Memorial Polyclinic inatarajia kujenga chuo cha HARMONY Kata ya Bonyokwa ili kiweze kuzalisha manesi  wa kisasa waweze kuisaidia Serikali katika kada ya sekta ya afya.


"Tunakushukuru Mbunge wetu wa Jimbo la Segerea   Bonah kuzindua Kituo chetu cha HARMONY hapa Bonyokwa tunaunga mkono juhudi zake  tumesogeza  huduma za afya karibu na wananchi  malengo yetu  tutafungua chuo cha afya ili tuzalishe manesi"alisema Mmari


Mmari alisema wakati wanamia Bonyokwa huduma za zahanati ni shida  mama wanasafiri umbali mrefu kutafuta Kituo cha afya  ndio wakapata ndoto ya kujenga Kituo hicho kikubwa chenye madaktari Bingwa  ambacho kinatoa huduma zote za afya zikiwemo za mama na Mtoto .


Mmari alisema Kituo chao cha afya taratibu za usajili wameanza mwezi Mei kimesajiliwa kina watumishi 21 kwa sasa.


Akielezea Changamoto alisema changamoto kubwa miundombinu ya Barabara ni mbovu kufika Harmony Hospitali tunaomba Mbunge Bonah na  Serikali itusaidie .


Kwa upande wake mgeni rasmi Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli alimpongeza Mkurugenzi wa Hospitali ya HARMONY kujenga Kituo cha afya kikubwa Bonyokwa.


Mbunge Bonah alisema Bonyokwa imezaliwa kutoka kata ya Kinyelezi ili kuwa kubwa ikagawanywa ikazaliwa Bonyokwa , Jimbo linatakiwa kuwa na  vituo vingi vya afya ili waweze kutoa huduma za afya karibu na wananchi.Akielezea miundumbinu ya Barabara alisema baadhi ya Barabara zipo chini ya TANRODS na zingine zipo katika usimamizi wa TARURA 


Bonah alisema kuhusu kero ya kipande cha Barabara mpaka kufika Hospitalini hapo amelichukua  ataitatua kwa haraka ili wagonjwa wakiingia na magari wasipate kero yoyote.

No comments:

Post a Comment