Thursday, 2 September 2021

DC LUSHOTO AHUDHURIA MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUMBULIMkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro leo Jumanne tarehe 31/08/2021 amehudhuria Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli uliofanyikia Shule ya Soni Sekondari na Kuwasisitiza Madiwani Kubuni Vyanzo vya Mapato na Kusimamia ioasavyo Utekelezaji wa Budget ya Halmashauri kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 na Kuhimiza Usimamizi kwenye Ukusangaji wa Mapato


Pia aliwasihi Watendaji wa Serikali; Watendaji wa Kata na Vijiji na Viongozi wa Kisiasa; Madiwani, Wenyeviti wa Serikali za Vijiji na Wenyeviti wa Vitongoji Kutotengeneza Migogoro na Kuacha tabia ya kujiona "Miungu Watu" na Kuwanyanyasa Wananchi kwa kuwalipisha faini bila Kuzingatia Kanuni za Halmashauri na Sheria Ndogo ndogo za Kijiji na kuacha mara moja Tabia ya Kujichukulia Sheria mkononi


Pia alisisitiza kuhusu Vikao vya Serikali za Vijiji Kufanyika kwa wakati kama Sheria inavyoelekeza na Viongozi Kujikita katika kutatua Kero za Wananchi kwenye maeneo yao na si kusubiri mpaka kero hizo zifikishwe na Wananchi Ofisi kwake.


Pia aliwataka Viongozi na Watendaji wa Serikali Kushirikiana kwa karibu na Wazazi, Wadau wa Elimu na Wanafunzi Kuhakikisha Wilaya ya Bumbuli inapaa zaidi Ki Elimu

No comments:

Post a Comment