Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha(CCM) chini ya  Mwenyekiti wake Joseph Massawe wamekasirishwa na uchafu wa kituo cha afya cha Moshono .


Aidha Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Sophia Mjema ametoa wiki moja kwa watoa huduma wa kituo hicho kusafisha mazingira ya kituo hicho  ikiwemo vyoo viwe visafi ili wananchi wapate huduma za afya 



Hayo yamejiri kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha ,huku Mwenyekiti wa chama hicho,Massawe  akimtaka Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ,John Pima kutotumia fedha za serikali katika kujenga maboma sehemu ambazo hazina uhitaji na kusababisha kuwa na majengo mengi ambayo na ni magofu bali wazielekeze fedha hizo kwenye maeneno yenye uhitaji.



"Ukitazama jengo hili limekamika muda mrefu lakini kwa sababu halitumiki na halina vifaa  limeanza kuchakaa,vyoo vichafu talaiesi chafu,huku nje kuchafu sasa mmeanza kujenga jengo lingine kule bado kule mmetumia fedha vibaya mmenunua mabati mengi mpaka mengine yamebaki sasa sijui mengine mtayapeleka wapi ila naagiza vyombo husika vije vichunguze hapa" .



"Kituo hiki kimejengwa kabla kile cha Murriet ukipita huko ndani tumekuta mafundi wanatindua wanaziba nyufa,huko ndani vyumba viwili ndivyo vinavyotoa huduma jengo limechaa na halijaanza kutumika,sitisheni Ujenzi wa ile ya mama na mtoto mkamilishe vifaa vya jengo hili kwanza Ili lianze kufanya kazi"



Ambapo Dc Mjema alichukizwa na uchafu wa kituo hicho na kutoa wiki moja kwa Mkurugenzi Pima usafi ufanywe kwani ni aibu kwa eneo hilo la afya kuwa chafu 


"mtajua mmnajipangaje nataka pawe pasafi,tukirudi kupakagua hapa kama watumishi mpo watano jipangeni fanyeni usafi hapa hiki ni kituo cha afya,nilikuwa nampango wa kukifunga kituo hiki kwa wiki moja ila nimeona nisitishe mfanye usafi hapa hamkujua anayekuja Mwenyekiti wa chama anakuja kama nyie hammuogopi mimi namuogopa,kile choo kichafu ukikiangalia utasema kimetumika miaka kumi"



Naye Diwani wa Kata ya Moshono Miriamu Kissawike aliomba kituo hicho kiboreshwe  ikiwemo kuongeza idadi ya watumishi huku Mwenyekiti wa chama kata ya Moshono,Siriel Mbise akisisitiza kutopepesa macho kwani kituo hicho bado hakina hadhi ya kutoa kutoa huduma za nje kwani ni kichafu



Ni kheri kusema kweli ituweke huru kituo hiki bado kabisa huduma ziboreshwe kwanini kituo cha afya ni kichafu namna hii, hii ni aibu



Naye matroni wa kituo hicho,Emerenciana Nivelle alisema wanafanya usafi wenyewe vyooni na kufyeka Makamu katika kituo hicho cha afya huku wakimaliza ndio watoe huduma za afya kuwa mama na mtoto ambapo ambapo idadi yao wapo watumishi watani wakiwemo madaktari wawili na manesi watatu

Share To:

Post A Comment: