Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson amezindua Taasisi isiyo ya kiserikali ijulikanayo Maryprisca Women Foundation(MWF) .


Uzinduzi  huo umefanyika  Jana katika ukumbi wa Sapanjo Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.


Kauli mbiu ya Taasisi hiyo ni"Tukue pamoja" yenye lengo la kusaidia masuala ya afya,elimu na uchumi.


Katika uzinduzi wa Taasisi hiyo Dkt Israel Mlabwa wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya(MZRH) alitoa elimu juu ya wanawake kujitokeza kupima afya zao hususani ugonjwa wa saratani ya matiti ili kuepuka madhara zaidi.


Kabla ya kuzindua asasi hiyo Dkt Tulia aliwapongeza wanawake wa Chunya kwa kumuunga mkono Mhandisi Maryprisca Mahundi.


"Naungana naye kuwashukuru wanawake kwa kumchagua Mahundi kuwawakilisha nakuomba uendelee hivyo hivyo"alisema Dkt Tulia.


Alimpongeza Mbunge wa Wanawake wa Mkoa wa Mbeya  Mhandisi Mahundi kwa kushiriki kuungana na Rais kutunza mazingira kwa kutoa majiko na miche ya miti.


Aidha amempongeza kwa kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwaanzishia mradi wa makalasha.


Amesihi wanawake wa Chunya kuacha maneno ili atulie Bungeni pia afanye kazi kwa utulivu kama kuna changamoto wasisite kumuelekeza wakishindwa yeye atamwelekeza.


Kwa kuonesha shukurani zake Mhandisi  Maryprisca Mahundi ametoa shilingi milioni kumi na moja kwa ajili ya kuanzisha mradi wa kiuchumi.

Share To:

Post A Comment: