Na. Angela Msimbira NSIMBO- KATAVI 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu alisema Serikali imejiwekea mkakati katika Sekta ya Elimu kwa kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi kwa waalimu wanaofanyakazi katika maeneo magumu na mbali kufikika

Aliyasema  hayo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara katika shule ya Sekondari ya Ugala River iliyopo katika kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi

Waziri Ummy alisema katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishia Serikali imejikita katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya waalimu wanaotoka mbali kupata maeneo ya kuishi.

“ Wapo waalimu ambao wanatoka mbali  mfano  mzuri ni hapa shule ya Sekondari Ugala River yupo mwalimu ametokea Kilimanjaro na kaamua kuja kufanyakazi katika Kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi, Ni wajibu wa Serikali na wananchi wa maeneo husika kuhakikisha wanaboresha mazingira  ili waweze kubaki muda mrefu  katika maeneo wanayofanyia kazi.” Alisema Mhe Ummy

Alisema Serikali inawatia moyo waalimu wote ambao wanafanyakazi katika maeneo magumu hasa katika kata za mbali na kuahidi kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samiah Hassan Suluhu itawekeza katika kuboresha mazingira ya watumishi nchini 

Kuhusu Nyumba za waalimu  katika Shule ya Sekondari Ugala RWaziri Ummy alisema katika kuunga mkono juhudi za wananchi Serikali itatoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya watumishi ambayo itachukua familia nne kwa pamoja. Lengo ni kuwatia moyo waalimu wanaofanyakazi katika maeneo ya mbali

Kuhusu ajira za waalimu wapya alisema Selikali ilitoa kipaombele kwa Halmashauri zenye maeneo yenye changamoto na maeneo ya mbali kufikika , jambo hili limetekelezwa  kwa asilimia 100 ambapo kwa shule ya Sekondari ya Ugala River  imepata waalimu wa Sayansi 3.

 Aidha, amesema Serikali ya awamu ya sita imeamua kujikita katika kuimarisha maeneo magumu kama  Halmashauri ya Nsimbo ambapo waalimu wapya wa Sayansi 26 wamepangwa katika Halmashauri hiyo








Share To:

Post A Comment: