Mkuu wa Mkoa Singida, Dk.Binilith Mahenge (kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru 2021 Mkuu  wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka katika Kijiji cha Naguru wilayani Bai baada ya kuhitimisha mbio zake mkoani humo leo. Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Singida ulitembelea miradi mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Sh.8 Bilioni.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge (katikati), akisoma taarifa ya mkoa wakati wa kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkoa wa Dodoma. Wengine kushoto kwa Dk. Mahenge ni Viongozi mbalimbali wa mkoa huo na kulia ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Singida..


Na Dotto Mwaibale, Singida


SERIKALI  Mkoa wa Singida chini ya Mkuu wa Mkoa huo Dk.Binilith Mahenge  leo asubuhi wamemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Anthony Mtaka baada ya kumaliza mbio zake mkoani humo.

Akisoma hotuba ya makabidhiano Dk. Mahenge alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Singida ulikibimbizwa umbali wa Kilometa 642.3 na jumla ya miradi 55 yenye  gharama ya zaidi ya Sh. 8 Bilioni iliwekewa mawe ya msingi, kuzinduliwa, kufunguliwa na kutembelewa katika sekta za maji, Elimu, Afya, Utawala Bora, Barabara, uwezeshwaji wa Wananchi Kiuchumi na program za mapambano ya UKIMWI, Maralia, Rushwa , mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya, Umuhimu wa Lishe na Matumizi sahihi ya Tehema, ambapo miradi yote ilikubaliwa na Mwenge huo wa Uhuru.

Mahenge aliwapongeza Vijana Sita Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa   kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiongozwa na  Luteni Josephine Mwambashi  na wenzake   Luteni Ramadhani  Msham, Luteni Geofrey  Aron, Luteni Mussa Mussa ,Coplo Rehema Haji na PTE  Dismas Mvula kwa kazi nzuri na kuaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kazi hiyo muhimu ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru na Ukaguzi wa Miradi kwa kina.

Aidha Mwenge wa Uhuru ulitoa ujumbe kwa Wananchi unaohusiana na Tehema chini ya kauli mbiu TEHEMA ni Msingi wa Taifa endelevu; Itumie kwa usahihi na Uwajibikaji pamoja na mapambano dhidi ya UKIMWI ,Maralia, Rushwa  , Mapambano dhidi Dawa za Kulevya  na umuhimu wa Lishe Bora na vijana sita walifafanua ujumbe wote.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa  LT Josephine Mwambashi akiwaaga wananchi wa Mkoa wa Singida wamempongeza  Mratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Singida Frederick Ndahani na Timu yake kwa Uratibu  mzuri  wa   mbio za Mwenge na kuwa ulikuwa mzuri na umesaidia kufanikisha mbio hizo mkoani humo.

Pia Mwambashi amewapongeza Wakuu wa Wilaya zote kwa usimamizi wa miradi uliosababisha miradi yote kukubaliwa. 

Mratibu wa Mwenge wa uhuru Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani ambaye pia ni Afisa Vijana wa Mkoa, amewashukuru wananchi, viongozi wa Serikali na Taasisi , Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama  vya Siasa wakiongozwa na Chama Tawala CCM  , Wakurugenzi, Makatibu Tawala, Timu ya Uratibu Mkoa,Waratibu wa Mwenge Wilaya na Wakuu wa Wilaya kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika Mbio za Mwenge wa uhuru  mkoani Singida.

Share To:

Post A Comment: