Mkuu wa Wilaya ya Singida Paskas Mulagiri akimkabidhi Mwenge wa Uhuru 2021 Mkuu wa wilaya Ikungi, Jerry Muro katika Kijiji cha Utaho baada ya kuhitimisha mbio zake wilayani humo leo. Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Ikungi unatarajiwa kupitia miradi mbalimbali yenye thamani ya Sh..2.9  Bilioni.

Mwenge wa Uhuru 2021 ukikimbizwa kabla ya kukabidhiwa Wilaya ya Ikungi.

Waratibu wa mbio za Mwenge Mkoa wa Singida wakiwa kwenye makabidhiano ya Mwenge huo.
Kurukaruka kwa furaha kukiendea wakati wa makabidhiano ya Mwenge huo.
Furaha tupu kwenye makabidhiano ya Mwenge huo
Mwenge wa Uhuru ukipokelewa.
Wanafunzi wakiwa kwenye mapokezi hayo.
Kurukaruka kwa furaha kukiendea wakati wa makabidhiano ya Mwenge huo, hawa ni wapambanaji kutoka Wilaya ya Singida.
Wananchi wakiwa kwenye makabidhiano ya Mwenge huo.
Wananchi wakiwa kwenye makabidhiano ya Mwenge huo.
Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yakiendelea. 
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama Wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye makabidhiano ya Mwenge huo.
Wananchi na Vijana wa Skauti wakiwa kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
Wanafunzi wakiwa kwenye mapokezi hayo.
Vijana wa Skauti wakimvika Skafu mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Mkuu wa wilaya Ikungi, Jerry Muro akimkabidhi zawadi Mkimbiza Mwenye wa Uhuru Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi.
Furaha tupu eneo la makabidhiano.
 


Na Dotto Mwaibale, Ikungi.


SERIKALI Wilayani Ikungi Mkoa wa Singida kwa kushirikiana na wananchi mapema leo asubuhi wameupokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Manispaa ya Singida ambapo utazindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye  thamani ya Sh. 2.9 Bilioni 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Mwenge huo na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Mulagiri katika Kijiji cha Utaho, Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro alisema  Mwenge huo utakimbizwa  kilometa 92.5 na kukagua miradi ya maendeleo.

Alisema Mwenge huo utaanza mbio zake kwa kutembelea Shule ya Msingi Semamba kukagua madarasa na mindombinu iliyojengwa kwa nguvu za wananchi na kuzindua klabu ya rushwa na kupanda miti.

Alitaja baadhi ya miradi mingine itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru kuwa ni Mradi wa ufyatuaji wa Matofali wa Kikundi cha Jitume Vijana, Mradi wa TEHAMA Sekondari ya Ikungi, Kuweka jiwe la msingi la Kituo cha Mafuta cha JMC, kukagua mifumo ya huduma ya afya Kituo cha afya Ikungi na kuzindua vyumba vya maabara za Sayansi Shule ya Sekondari ya Unyahati.

Muro alitumia nafasi hiyo kuwatambulisha viongozi mbalimbali waliokuwepo kuupokea Mwenge wa Uhuru akiwepo Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Winfrida Funto ambaye alikuwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM), Wajumbe wa Kamati ya Siasa na Sekretarieti, Wabunge, Wananchi, Viongozi wa dini, Watumishi wa Halmashauri hiyo Madiwani na wanafunzi.

Share To:

Post A Comment: