Jane Edward, Arusha

Baadhi ya wananchi wa halmashauri ya jiji la Arusha, wameilalamikia mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira jiji la Arusha (Auwsa)kwa kile kinachodaiwa kuwa bili ya maji kuwa kubwa tofauti na matumizi halisi.


Wakizungumza na waandishi wa habari wananchi hao,Agnes Shirima wamesema kuwa ,wasoma mita wa mamlaka hiyo wamekuwa wakiandikia wateja bili kubwa na wakati mwingine kusoma mita bila mhusika kuwepo na hivyo kushindwa kuuliza maswali.


"Unakuta Mwenye nyumba ameenda kazini ule muda msoma mita anapokuja anasoma mita na kuandika bili ya maji bila mhusika kuridhia hali inayotupa wakati mgumu wa kulipa bili husika"alisema Agnes.



Akijibu malalamiko hayo, Meneja wa mahusiano ya uuma kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira,Masoud Katiba amesema kuwa dawati lao la huduma kwa wateja lipo wazi na kama wateja wanaona kuna changamoto ya usomaji mita wao wako tayari kufika Nyumbani kwa mteja kwaajili ya kubaini tatizo.


"Kesi kama hizo ni chache sana kama zipo na kwamba mteja anapoona kuna hizo changamoto apige simu namba ya huduma kwa wateja ili wataalamu wafike nyumbani kwake na kubaini tatizo na kulifanyia kazi" Alisema Katiba


Katiba ameongeza kuwa nia ya mamlaka hiyo ni kuhakikisha inahudumia wateja wake kikamilifu bila kuwa na malalamiko yoyote na hivyo wananchi wote wa jiji la Arusha wametakiwa kuonyesha ushirikiano ili kuendana na kasi ya huduma bora inayotakiwa.


Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: