Mwakilishi wa Mkurugenzi wa  Mfuko wa Maendeleo wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) kutoka Makao Makuu,, Peter Lwanda akisoma taarifa ya TASAF Awamu ya Tatu Sehemu ya  Pili wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jwilayani humo mkoani Singida jana..

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa, akizungumza katika uzinduzi huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Manyoni, Jumanne Mgalaza, akitoa mkazo kkwa Madiwani kwenda  kuhakikisha walengwa ndio wanaonufaika na mpango huo.

Wakuu wa Vitengo Ngazi ya Halmashauri na wa idara wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa  Mfuko wa Maendeleo wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) kutoka Makao Makuu,, Peter Lwanda.
Uzinduzi ukiendelea.
Wataalamu kutoka TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Manyoni wakati wa uzinduzi huo.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Manyoni ikiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TASAF na Viongozi wa Halmashauri.
Uzinduzi ukiendelea.
Madiwani  wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TASAF na Viongozi wa Halmashauri.ya Manyoni.
Viongozi wakiwa meza kuu.

Wawezeshaji  wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TASAF na Viongozi wa Halmashauri.ya Manyoni.



 Alinikisya Humbo na Dotto Mwaibale, Manyoni.

MKUU wa Wilaya ya Manyoni,  Rahabu Mwagisa amezindua kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF.

Akizungumza na wawezeshaji waliofika ili kupata mafunzo hayo Mwagisa alisema kuwa madhumuni ya mpango wa kipindi cha pili ni kuwezesha Kaya za walengwa kutumia fursa za kuongeza kipato, kuboresha huduma za jamii na kiuchumi, na kuwezesha katika maendeleo ya Watoto ambao ni raslmali watu.

Mwagisa ameishukuru Serikali ya awamu ya sita na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan kwa kuendelea kuuborehsa mpango huu wa TASAF na kuona tija ya kuzisaidia kaya hizo maskini ili ziweze kunufaika. 

Aidha amewataka wawezeshaji kuzingatia mafunzo watakayopatiwa na wataalamu  na kwamba wazingatie na kuhakikisha mpango unawafikia walengwa pindi watakapokuwa uko vijijini na wafuate miongozo iliyowekwa na kuwa makini.

“Nitoe rai kwenu wote kuzingatia mafunzo haya na kuhakikisha mnatekeleza mpango kazi huu mtakapokuwa huko vijijini basi mkazingazitie miongozo mliyopewa na kuhakikisha walengwa wote wananufaika na mpango huu”alisema  Mwagisa.

Akisoma hotuba mbele ya Washiriki wa Mafunzo hayo Afisa  Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA ) wa TASAF,  Peter Lwanda amesema kuwa  kipindi cha awamu ya tatu ya mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAFIII) kinatekelezwa katika 
Halmashauri zote 184 za Tanzania Bara na Wilaya zote za Zanzibar..

Aidha ameongeza kuwa kipindi cha pili cha awamu ya tatu TASAF kitafika kaya milioni moja laki nne na nusu zenye jumla ya watu zaidi ya million saba nchi nzima.

“Mkazo mkubwa katika kipindi hiki cha pili umewekwa katika kuwezesha kaya zitakazoandikishwa kwenye mpango kufanya kazi ili kuongeza kipato”alisema Lwanda.

Lwanda alisema kuwa kipindi hiki cha pili kitahakikisha kwamba huduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa ili kutoa huduma na kuendeleza rasilmali Watoto hususani katika upatikanaji wa Elimu na Afya.

Akitaja walengwa wa awamu hii ya pili Lwanda amesema kuwa ni kaya zinazoishi katika hali duni kwenye Vijiji,Mitaa na, Shehia na kwamba wanufaika ndani ya kaya ni Watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanaohudhuria kliniki,wanafunzi wa  shule za awali,shule za msingi na shule za sekondari,mama wajawazito na mwanakaya mwenye ulemavu.

“Niseme tu kwamba mpango huu unatoa ruzuku za aina mbili,ruzuku ya msingi na ruzuku ya masharti kwa wale ambao wanatakiwa kwenda shuleni na Watoto wanaohudhuria kliniki”alisema Lwanda.

Hata hivyo Lwanda alisema kuwa kuna ajira mpya ambazo pia zitaweza kuwanufaisha mwanakaya mmoja ambaye ataonekana kuwa na uwezo wa kufanya kazi. 

Lwanda  amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji Charls Fuss kwa kutoa wawewzeshaji wengi na hasa ngazi ya kata ili kuja kushiriki mpango kazi huo.

Naye Mratibu wa TASAF Wilaya ya Manyoni Kenenan Kidanka ameshukuru wataalamu hao kwa kuweza kuiweka Wilaya ya Manyoni katika mpango huu kwa awamu nyingine tena na kuwaweka watu wenye ulemavu katika mpango huo.

Kidanka alisema  kuwa watahakikisha wanaweka usimamizi na mkazo zaidi ili kuhakikisha mpango unawafikia walengwa katika vijiji vyote na kaya zote.

“Nitoe shukrani kwa wataalamu kuweza  kuiweka Manyoni katika mpango na awamu hii na hasa niwashukuru pia kwa kuwakumbuka na watu wenye ulemavu nao kuingia kwenye mpango huu tunashukuru sana”alisema Kidanka.
 

Share To:

Post A Comment: