Mkurugenzi wa Makumbusho ya Viumbe Hai Iliyopo jijini  Arusha Dkt. Christina Ngereza.



Na Dotto Mwaibale  


MAKUMBUSHO  ya Taifa ya Tanzania yanatarajia kuungana na maakumbusho zote duniani katika kuadhimisha Siku ya Makumbusho Dunia itakayo adhimishwa  Mei 18 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini  Arusha, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Viumbe Hai Iliyopo jijini  Arusha Dkt. Christina Ngereza alimesema katika Maadhimisho hayo ya mwaka huu Tanzania itaungana na nchi zaidi ya 158 duniani kuadhimisha siku hiyo chini ya kauli mbiu Mstakabali wa Makumbusho 'The Future of Museums: Recover and Re imagine’

Akizungumzia kuhusu kuadhimisha kumbukizi hizo Makumbusho ya Taifa  kupitia kituo chake cha Makumbusho ya Taifa ya Elimu Viumbe Hai pamoja na mambo mengine wamejipanga kutoa elimu ya kuwajengea uelewa wananchi juu ya kutembelea makumbusho  kama sehemu ya kupata elimu na burdani kuhusu urithi wa nchi wa kale na wa Sasa wa Asili Mazingira, Utamaduni Sayansi, Teknolojia na Historia.

Dkt. Ngereza alisema siku hiyo makumbusho zote zitakuwa wazi hivyo ni vema Watanzania wafike kwa wingi kupata elimu na mambo muhimu ambayo yatafanyika katika makumbusho zote. 

" Lengo la siku hii maalum ni kujenga uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa Makumbusho katika Nyanja mbalimbali za maendeleo." alisema Ngereza.

Alisema katika kuadhimisha siku hiyo muhimu kila mwaka Jumuiya ya Kimakumbusho ya Dunia  (ICOM) huchagua mada katika kuadhimisha siku ya Makumbusho  Duniani ambayo ni agenda  muhimu katika jamii. 

Alitaja elimu itakayotolewa kuwa ni  Makumbusho ni nini, Umuhimu wa Makumbusho katika maendelo ya nchi na haja ya kuwa na Makumbusho nyingi mbalimbali Tanzania. 


Share To:

Post A Comment: