Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. William Ole Nasha (Mb) akiwasili makao makuu ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuongoza wizara hiyo, Leo Aprili 19, 2021 Dar es salaam

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. William Ole Nasha (Mb)akitambulishwa wafanyakazi wa taasisi mbalimbali waliofika kwenye ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ikiwa ni ziara ya kwanza kwenye kituo hiki tangu alipoteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suruhu Hassan kuongoza wizara hii, Leo Aprili 19, 2021 Dar es salaam ambapo amezungumza na watendaji wa Taasisi mbalimbali za serikali.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. William Ole Nasha (Mb)akitambulishwa wafanyakazi wa taasisi mbalimbali waliofika kwenye ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ikiwa ni ziara ya kwanza kwenye kituo hiki tangu alipoteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suruhu Hassan kuongoza wizara hii, Leo Aprili 19, 2021 Dar es salaam ambapo amezungumza na watendaji wa Taasisi mbalimbali za serikali.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. William Ole Nasha (Mb)akiakielekea kwenye  ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ikiwa ni ziara ya kwanza kwenye kituo hiki tangu alipoteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suruhu Hassan kuongoza wizara hii, Leo Aprili 19, 2021 Dar es salaam ambapo amezungumza na watendaji wa Taasisi mbalimbali za serikali katikati ni  Katibu Mkuu Ofisi ya waziri mkuu Uwekezaji Prof. Godius Kahyarara na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Bw. Mafutah Bunini.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. William Ole Nasha (Mb) akisaini kwenye kitabu cha wageni kwenye ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ikiwa ni ziara ya kwanza kwenye kituo hiki tangu alipoteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suruhu Hassan kuongoza wizara hii, Leo Aprili 19, 2021 Dar es salaam

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. William Ole Nasha (Mb) akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya waziri mkuu Uwekezaji Prof. Godius Kahyarara na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Bw. Mafutah Bunini alipowasili kwenye ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ikiwa ni ziara ya kwanza kwenye kituo hiki tangu alipoteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suruhu Hassan kuongoza wizara hii, Leo Aprili 19, 2021 Dar es salaam

Baadhi ya watendaji wa taasisi mbalimbali wakiwa katika ofisi za kituo cha uwekezaji TIC leo.

  

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. William Ole Nasha (Mb) akizungumza katika kikao hicho kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya waziri mkuu Uwekezaji Prof. Godius Kahyarara.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. William Ole Nasha (Mb) akimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya waziri mkuu Uwekezaji Prof. Godius Kahyarara wakati alipokuwa akizungumza na watendaji katika kikao hicho.

...............................................

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. William Ole Nasha (Mb) amewahakikishia wawekezaji kuwa serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) imejipanga kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa kuwaondolea vikwazo na changamoto zinazowakabili wawekezaji.

 Naibu Waziri Mhe. Ole Nasha ameyasema hayo leo Aprili 19, 2021  Dar es Salaam katika kikao kazi kilichohusisha Menejimenti ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pia Wakurugezi na wawakikishi wa Wakurugenzi kutoka Taasisi za Bohari ya Dawa (MSD), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kilichokuwa na lengo la kujadili kwa pamoja namna ya kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuweka mpango kazi ili kurahisisha uwekezaji thabiti na wenye tija kwa manufaa ya Watanzania, kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Godius Kahyarara.

  Aidha, Naibu Waziri Mhe. Ole Nasha amesisitiza kuwa Wizara imejipanga kusimamia miradi yote ambayo imeanza kutekelezwa na Serikali na taasisi ili kuhakikisha inaisha kwa wakati ikiwa ni moja ya maelekezo yaliyotolewa kwa Wizara hiyo ambayo wanatakiwa kisimamiwa.

 “Mheshimiwa Rais katika hotuba zake amekuwa akisisitiza kwamba miradi ambayo Serikali imeanza kutekelezwa inapaswa kukamilika kwa wakati, tabia ya kuwa na miradi ambayo inaenda miaka na miaka bila kumalizika Mheshimiwa Rais hataki ndio maana leo hii tumeanza utaratibu kama Wizara iliyopewa jukumu la kuratibu uwekezaji nchini kujua miradi hiyo na kuwa na kanzidata ya miradi yote ya uwekezaji pamoja na wawekezaji ili tuweze kufahamu na kusimamia hii itasaidia sana kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na ndio maana tumekutana na MSD, NSSF na NHC”

 Naibu Waziri Mhe. Ole Nasha ameongeza kuwa Wizara itaendelea kukutana na taasisi mbalimbali ili kuwaunganisha na Kituo cha uwekezaji Tanzania na kujadiliana kwa pamoja ni kwa namna gani wataweza kuboresha uwekezaji kwa kuzifahamu na kuzitatua changamoto mbalimbali kama ni za kisheria au kisera ziweze kurekebishwa kupitia Taasisi hizo ambazo zinatekeleza miradi hiyo.

 Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Prof. Godius Kahyarara amesema kuwa Wizara imejipanga kutekeleza maagizo na maelekezo yote yaliyotolewa na yanayoendelea kutolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto na vikwazo vinavyowakabili wawekezaji katika maeneo mbalimbali kama vile upatikanaji wa vibali, muda wa kupata vibali na maswala ya ardhi na mengineyo.

 Prof. Godius Kahyarara ameeleza kuwa Serikali ipo mbioni kubadilisha sheria ya uwekezaji kwahiyo hiki ni kipindi cha kupata maoni kwa wanaohusika kusimamia uwekezaji ikiwemo Taasisi za umma lakini amesisitiza kuwa kwa kuunganisha nguvu pamoja na Taasisi za umma wataweza kuratibu na kusaidia kuzikabili changamoto hizo.

 Kikao kazi hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kikiongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. William Ole Nasha (Mb).

Share To:

msumbanews

Post A Comment: