Naibu Waziri wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akimsikiliza kwa makini mtendaji mkuu wa kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd (PCT) ndugu John Power.

Naibu Waziri wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akisaini kitabu cha cha wageni mara baada ya kufika katika kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd (PCT).

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi ndugu Jamhuri Devid Willium akizungumza wakati wa kikao kilichofanyika katika kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd (PCT), pembeni ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe.

Mtendaji mkuu wa kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd (PCT) ndugu John Power akizungumza katika kikao kujadili changamoto za kiwanda, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi ndugu Jamhuri Devid Willium na aliyekaa katikati ni Naibu Waziri wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe.

Shamba la pareto lililopo katika kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd (PCT).

Naibu Waziri wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akikagua kiwanda cha kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd (PCT) kuona uzalishaji wa pareto unaoendelea kiwandani hapo.

Naibu Waziri wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akiangalia zao la Sabadilla ambalo linafanyiwa utafiti na kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd (PCT) zao hili linatengeneza bidhaa zilezile ambazo pareto inatengeneza.

Zao la Sabadilla linalofanyiwa utafiti na kiwanda kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd (PCT).


Na.Mwaandishi wetu,Mafinga

 
Naibu waziri wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd (PCT) kilichopo Mafinga Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa na kujionea shughuli za kiwanda zikiendelea za uchakati wa pareto.
Mhe. Kigahe amefanya ziara hiyo leo tarehe 24 Aprili, 2021 katika kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha tani 5000 kwa mwaka ambapo uzalishaji wake kwa sasa ni tani 300 na hii imetokana na changamoto ya upatikanaji wa malighafi ambayo ni pareto. 


Kiwanda cha PCT kwa sasa kimeajiri wafanyakazi wa kudumu 146 na wafanyakazi wasio wa kudumu wako zaidi ya 100 ambapo masoko ya kiwanda hiki kwa kiasi kikubwa zaidi ya asilimia 90 wanauza nchini Marekani ndipo kuna soko kubwa, masoko mengine ni Japan na India. 


“lengo la ziara yangu ni kutembelea kiwanda hiki na kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo ili kuhakikisha zinatatuliwa kwa wakati na kutoa fursa kwa wakulima kulima kwa kiasi kikubwa kwani soko lipo katika kiwanda hiki, serikali inahitaji kiwanda hiki kiongeze uzalishaji ili kuongeza ajira na kodi kwa serikali lakini pia kipato cha mwananchi mmoja mmoja”amesema Mhe. Kigahe. 


Mhe. Kigahe ameongeza kuwa serikali inahitaji kuwa na viwanda vingi vinavyochakata mazao ya kilimo na kuongeza thamani kabla ya kuuza nje ya nchi ili kuongeza fedha za kigeni na kukuza pato la taifa hivyo mkazo mkubwa ni katika kuhakikisha serikali inalinda viwanda vya ndani hasa vinavyochakata mazao ya kilimo. 


Mkuu wa Wilaya ya Mufindi ndugu Jamhuri Devid Willium amempongeza Mhe. Naibu waziri kwa kutembelea kiwanda hicho kwani kiwanda hiki kina historia kubwa ya nchi yetu, wakulima wa Mufindi ni wakulima wazuri wa pareto kwa kutumia vyama vya ushirika AMCOS ambao wanasaidia pia katika upatikanaji wa pembejeo. 


Mhe. Jamhuri amesema kuwa walanguzi wa zao la pareto wamekuwa wakidhibitiwa kwa nguvu zote katika wilaya ya Mufindi kwani walanguzi hao wanakwepa kodi, wanawapunja wakulima katika mizani, hawalipi kodi ya halmashauri na serikali ya wilaya. 


Juhudi kubwa zimekuwa zikifanywa na kiwanda cha PCT ya kutoa mbegu bora bure kwa wakulima, kutoa mafunzo ya kilimo bora na vikaushio vya pareto katika kurahisisha kukausha pareto, bado kumekuwa na changamoto kwa wakulima kutokuwekeza katika kilimo cha pareto. 


Kiwanda cha PCT kipo katika mpango wa kuanzisha kilimo cha kisasa cha (Block farming) ambayo itakuwa suluhisho kwa wakulima kulima shamba kubwa wakisaidiwa pembejeo na vitendea kazi pamoja na huduma nyinginezo za ugani. 


Mhe. Exaud Kigahe ametembelea pia shamba la zao la SABADILLA ambalo bado liko katika utafiti kwa mwaka wa nne sasa na karibu itatolewa tathimini ya utafiti huo ambapo zao hili litasaidia kuongeza mazao mengine mbadala ili kutoa fursa kwa wakulima kulima mazao mengine kwa gharama nafuu zaidi.

 Zao la SABADILLA ni zao ambalo linatengeneza bidhaa zilezile ambazo pareto inatengeneza. 


Kwa upande wake Mhasibu Mkuu wa kiwanda cha PCT ndugu Gerald Joseph ameshukuru sana kwa ujio wa Mhe. Naibu waziri kwani wamepata fursa ya kutosha kueleza changamoto zao na waziri amehaidi kuzifanyia kazi kwa haraka katika kusaidia kuongeza uzalishaji wa pareto ili kuhamasisha wakulima kuongeza ulimaji wa pareto. 

Kind regards Alex Mathias Sonna Chief Editor Fullshangwe Blog Email:alexsonna915@gmail.com Cellphone:+255653257072 Twitter:@ALEXSonna Instagram:@sonnaalex

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: