Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na viongozi na watendaji wa sekta ya ardhi katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Magu wakati wa ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Mwanza tarehe 2 Machi 2021.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akioneshwa ramani ya mradi wa upimaji katika eneo la Kisesa wilaya ya Magu mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi tarehe 2 Machi 2021.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Kisesa katika wilaya ya Magu baada ya kugawa hati za ardhi wakati wa ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Mwanza tarehe 2 Machi 2021.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akielekea kukagua mradi wa upimaji katika eneo la Kisesa wilaya ya Magu wakati wa ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Mwanza tarehe 2 Machi 2021. Kulia kwa Waziri Lukuvi ni Mkuu wa wilaya ya Magu Salum Kalli.

Na Munir Shemweta, MAGU

Waziri wa Ardhi Mhe William Lukuvi amezitaka Halmashauri kutambua maeneo yote ya vijiji yanayochipukia kuwa miji na kuyapangia mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Lukuvi amesema hayo leo tarehe 2 Machi 2021 wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Magu akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Mwanza.

Alisema, baada ya serikali ya awamu ya tano kuweka jitihada kubwa katika kusambaza umeme vijijini kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini (REA) sasa vijiji vinaishi kimji na maisha yamebadilika ambapo vijiji vingi vimekuwa miji.

Aliongeza kwa kusema kuwa, ni vizuri halmashauri ambazo ni mamlaka ya upangaji kuangalia ni vijiji gani vimechipukia kimji na kuvipangia matumizi bora ya ardhi yatakayoainisha shughuli kama vile kilimo, ufugaji na kusisitiza kuwa wasipofanya upangaji mapema watashindwa kuvipanga baadaye.

Hata hivyo, alisema katika maeneo ambayo vijiji vyake havina sifa ya kuchipukia kuwa miji halmashauri isimamie ujenzi wa makazi katika vijiji hivyo kwa kuviwekea utaratibu wa kujenga nyumba kwa mpangilio ulio bora.

"Kazi ya kupanga vijiji ni ya halmashauri kama ambavyo mnapanga kujenga madarasa 5 kwa mwaka katika halmashauri basi muweke malengo ya kupanga vijiji 10 kwa mwaka" alisema Lukuvi.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alikagua mradi wa upimaji ardhi eneo la Kisesa katika halmashauri ya wilaya ya Magu na kuitaka halmashauri hiyo kuwatumia watendaji wa serikali katika kazi ya upimaji badala ya kutegemea makampuni ya upimaji aliyoyaeleza kuwa wakati mwingine yamekuwa yakiwatoza fedha nyingi wananchi.

"Tumieni watumishi walio katika halmashauri kushambulia kupima maeneo mbalimbali na vifaa vya upimaji vipo vya kutosha katika ofisi za ardhi za mikoa" alisema Lukuvi.

Hata hivyo, alisema kama halmashauri zitashindwa kupima maeneo kutokana na uchache wa watumishi zichukue wanafunzi wa vyuo vya ardhi ambapo aliagiza kazi zote zilizoshindwa kufanywa na makampuni ya upimaji sasa zifanywe na watendaji wa sekta ya ardhi wa serikali.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mwanza Eliah Kamyanda alisema kuwa, mkoa wa Mwanza ni moja ya mikoa 16 iliyopewa fedha na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya programau ya kuwezesha kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kwenye maeneo mbalimbali nchini na programu hiyo katika eneo la kisesa na Bujora itapima takriban viwanja 3000.

Waziri Lukuvi alizitaka halmashauri kuelewa kwamba zina mamlaka ya upangaji katika maeneo mbalimbali na zinatakiwa kujua umuhimu wa kupanga na kupima na kumilikisha ardhi kwa wananchi.

" Halmashauri ziisaidie serikali kutengeneza walipa kodi, hawa 3000 ambao Wizara ya Ardhi imetoa shilingi milioni 220 kwa ajili ya mradi wa kupima na kumilikisha ardhi, nimeelezwa ndani ya siku 90 wamiliki wake watakuwa wamemilikishwa, nataka mwaka mmoja mpime viwanja 12,000 katika kata za Bujora na Kisesa" alisema Lukuv
Share To:

Post A Comment: