Teddy Kilanga


ARUSHA


Wadau wa Sekta ya Asasi za kiraia  kanda ya kaskazini wametoa salamu za pole kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania,Dkt.Magufuli kilichotokea mnamo machi 17 na kuzikwa machi 26.


Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Pingo's wawakilishi wa asasi za kiraia kanda ya kaskazini alisema wao kama asasi za kiraia watamkumbuka ,Dkt. Magufuli kwa jitihada zake alizofanya katika kuleta maendeleo ikiwemo kupiga vita rushwa na ufisadi,kuboresha miundombinu,huduma za kijamii pamoja na kuweka nidhamu ya utumishi wa umma.


"Tunatambua kuwa  tangu mwaka1995 alipochaguliwa kuwa mbunge na baadaye kuwa naibu waziri pamoja na waziri wa katika wizara tofauti tofauti hadi kufikia nafasi ya Rais,Hayati,Dkt.Magufuli alikuwa mstari wa mbele katika kupinga rushwa na kuleta uwajibikaji  katika idara za umma pamoja na kupiga vita dhidi ya umaskini na uboreshaji wa miundo mbinu,"alisema.


Mwakilishi kutoka asasi ya  jumuiko la maliasili,Magreth Mollel alisema kabla ya uchaguzi mkuu  wa mwaka 2015 kulikuwa na kilio kikubwa cha wadau wa asasi za kiraia kuhusu mambo kadhaa ikiwemo kukosekana kwa uadilifu katika sekta ya umma,utawala wa sheria,katiba mpya,haki za kibinadamu,umaskini miongoni mwa jamii pamoja na changamoto katika sekta mbalimbali kama elimu,afya,miundombinu na nishati.


"Hayati Rais Magufuli alijitahidi sana kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ambazo zilikuwa zinaendelea kufanyiwa kazi hadi umauti unamkuta,lakini kuna mambo muhimu yaliyofanyika au kukamilika katika kipindi cha uongozi wake kama vile kukuza uchumi wa Kitaifa pamoja na mikutano ya kila mwaka ya wakurugenzi wa Azaki ambapo wageni rasmi wamekuwa ni mawaziri pamoja na viongozi wengine wa serikali.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa asasi ya kirai ya utetezi wa haki za kibinadamu (Cilao)Charles Odero alisema wanampongeza Rais.Suluhu Hassan  kwa kupata nafasi ya kuongoza nchi hivyo wanaimani naye  kwa utendaji wa kazi katika kipindi chote cha uongozi wake kutokana nafasi mbalimbali za uongozi  alizowai kushika katika kipindi cha nyuma.


"Katika nafasi mbalimbali alizoshika  Rais.Samia Suluhu Hassan amekua mstari wa mbele kufanya kazi  na wadau wa asasi za kiraia katika kuhakikisha mambo mbalimbali muhimu kwa jamii yanatekelezwa  miongoni mwa maeneo muhimu aliyosimamia moja kwa moja ni pamoja na uboreshaji wa vituo vya afya na huduma muhimu,huduma ya maji maarufu kampeni ya kumtua mama ndoo,kuboresha hali ya lishe kwa akina mama wajawazito na watoto waliochini ya umri wa  miaka mitano,"alisema Odero.


Alisema amekuwa mstari wa mbele pia kwa vijana balehe , wazee na kuzindua mradi wa kutokomeza unyanyasaji wa wanawake na watoto masokoni pamoja na kupambania kumuinua mwanamke kiuchumi na kuwa mlezi wa mabaraza ya kumuinua mwanamke kiuchumi.


Amani Liazer kutoka shirika lisilo la kiserikali la kifugaji jamii ya kimasai,alisema katika kushiriki mikutano ya Azaki na kutoa ushirikiano kwenye kazi mbalimbali zinazoandaliwa  na Asasi za kiraia wanapata matumaini na nguvu kubwa kuimarisha utoaji huduma mbalimbali kwa jamii ikiwa baadhi ya maeneo ambayo wanaendelea kuboresha  na kufanya kazi karibu zaidi na serikali kuhakikisha wanachangia katika mafanikio ya Rais Suluhu Hassan.


"Kuendelea kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi kwa fedha zinazotumika katika miradi mbalimbali ambayo taarifa iliyotolewa na asasi za kiraia katika wiki ya asasi za kiraia novemba 7 mwaka2019,mashirika 16 yaliyofanyiwa utafiti yalionyesha yameingiza nchini takribani sh.bilioni 236 katika kipindi cha miaka mitatu,"alisema




Mkurugenzi mtendaji wa taaasisi ya utetezi jamii za pembezoni kupitia vyombo vya habari (Maipac)Mussa Juma alisema wanamuomba Rais,Samia Suluhu kuwa kupata fursa ya kukutana na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa muda atakayeupanga  ili kuweza kuwapa mwelekeo wake kwa lengo la kuboresha tasnia ya Utendaji kazi wa NGOs mbalimbali.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: