Raisa Said, Kilindi 

KATIKA kukabiliana na tatizo la kuongezeka kwa tatizo la vifo vya watoto njti wilayani Kilindi, wilaya hiyo imeanza kutekeleza mikakati mahususi ya kukabiliana na tatizo hilo.


Kwa mujibu wa  DK Daniel Chochole  ambaye ni Mganga Mkuu wa wilaya  ya kilindi ,  amesema  wilaya hiyo  haina sehemu maalum ya kuhifadhia watoto njiti hivyo imeandaa chumba maalum kwa ajili hiyo.


Akizungumza katika mahojiano maalum, Dk  Chochole alisema kuwa wilaya imekwisha andaa zaidi ya Sh milioni saba (7) kwa ajili ya kufanya ukarabati wa chumba hicho ili kukitayarisha kwa kazi hiyo kama vile kuweka vifaa kwa ajili ya kuongeza joto katika chumba.


Hata hivyo Mganga Mkuu huyo, alisema kuwa walikwisha peleka oda yao kwa ajili ya kupata vifaa katika Bohari ya Dawa lakini alieleza kuwa kuna changamoto ya upatikanaji wa vifaa hivyo.  


Akizungumzia tatizo alisema kuwa hakuna takwimu hivi sasa zinaonyesha ni vifo vingapi vimetokea kwa sababu ule mfumo wa kuweka kumbukumbu sasa hivi haupo. Hata hvyo, alisema kuwa tatizo hilo ni kubwa.


Alisema kuwa wanaendelea kuwapa elimu wakina mama wajawazito juu ya umuhimu wa kwenda kliniki mapema ambapo kama kuna shida yoyote ambayo inaweza kusababisha kuzaa mtoto njiti linabainishwa.


Alisema sababu kuna matatizo mengi yanayosabisha kina mama kuzaa watoto njiti kama vile uvimbe kwenye kizazi, malaria, upungufu wa damu. “Katika mazingira yetu malaria na upungufu wa damu. Alisema tatizo la upungufu wa damu linaweza kusababishwa na lishe duni,” alisema Dk Chochole.


Alisema kuwa idara ya afya imekuwa ikitoa elimu maluum kwa kina mama juu ya nmna bora ya kuhudumia watoto njiti ikiwa ni pamoja na kumkumbatia mtoto kifuni kwa muda mrefu na kumwambukiza joto, njia ambayo maarufu kama ‘kangaroo’.


Alitoa wito kwa wazazi na kusema kuwa pindi wanaposhika ujauzito waanze kliniki mara moja. Alisema iuwa saabu za kuzaa watoto niti zinaweza kuzuilika wakatia wa ujauzito.


Nchini Tanzania, takwimu zinaonyesha asilimia 13 ya watoto huzaliwa wakiwa na uzito pungufu ambao huchangia kwa asilimia 86 ya vifo vya wachanga.


Ripoti ihiyo inasema tatizo linalochangia kusababisha vifo vya watoto hao linakadiriwa kufikia asilimia 27 ya vifo hivyo, ni pamoja na mtoto kuzaliwa njiti, maradhi ya vimelea vya bakteria, matatizo ya kupumua na kuvuja damu.


Kwa mwaka 2019 takwimu zinaonyesha kwa mkoa wa tanga  ni wastani  wa watoto njiti  60 mpaka 80 huzaliwa kila mwaka.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: