Na Heri Shaaban


DIWANI wa Kata ya Kipawa Aidani Kwezi amekutana na Wazazi wa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ilala katika kikao cha Elimu. 



Akizungimza katika kikao cha sekta ya elimu shuleni hapo Diwani Aidan aliwataka Wazazi kushirikiana na Walimu pamoja na kufatilia maendeleo ya watoto wao ili kukuza taaluma shuleni hapo. 


"Nawaomba wazazi tushirikiane na Walimu sambamba na kufatilia maendeleo ya Watoto wetu shule ili waweze kufanya vizuri darasani shule zetu ziongeze ufaulu "alisema Aidan. 


Diwani Aidani alisema katika kikao hicho leo walikutana na wazazi wa kidato cha pili na kidato cha tatu na kupanga mikakati ya kukuza elimu ambapo wazazi walikubaliana kwa kushirikiana na Walimu. 



Aliwataka Wanafunzi wa Kata ya kipawa kuzingatia elimu aina mwisho wasome kwa bidii ili waweze kuwa viongozi wa baadae. 



Diwani Aidani alisema mikakati hiyo ya Elimu ni katika kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli mpango wa Elimu bure. 


Alisema Taifa lolote lazima liwe na Maendeleo lazima watu wake wasome hivyo anaweka mikakati hiyo ya elimu kuakikisha Kipawa inafanya vizuri sekta ya Elimu. 


Share To:

Post A Comment: