Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 2, 2021 ameanza ziara ya kikazi Mkoa wa Ruvuma kwa kukagua ukarabati wa majengo ya  Shule ya Sekondari ya Tunduru.


Akiongea baada ya ukaguzi huo Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia lengo ni kuwawezesha watoto wa kitanzania kupata elimu bora na kutimiza ndoto zao.


Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkoani humo Gasper Balyomi kupeleka gari katika Shule  ambayo kwa sasa haina gari  ili kuwahudumia walimu na wanafunzi na kurahisisha utekelezaji wa majukumu shuleni hapo.

Share To:

Post A Comment: