Mwanamitindo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Flaviana Matata akizungumza na wanafunzi,walimu pamoja na wazazi wa Shule ya Msingi Msinune wakati wa kutoa msaada wa vifaa vya shule ikiwa ni utaratibu aliouweka kama mlezi shule hiyo iliyopo mtaa wa Msinune Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete akizungumza na uongozi wa Taasisi ya Flaviana Matata, wanafunzi, walimu pamoja na uongozi wa Shule ya Msingi ya Msinune wakati wa kugawa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi na vifaa vya kufundishia kwa walimu vitakavyotumika kwa mwaka mzima vilivyotolewa na Taasisi ya Flaviana Matata.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Usinune Alex Lugaigila akitoa historia ya shule hiyo ilivyodhaminiwa na  Taasisi ya Flaviana Matata kuanzia mwaka 2016 hadi 2021 wakati wa zoezi la kugawa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi na vifaa vya kufundishia kwa walimu vitakavyotumika kwa mwaka mzima vilivyotolewa na Taasisi hiyo leo.

Mwanamitindo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Flaviana Matata, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete, viongozi wa Tarafa pamoja na viongozi wa Shule wakigawa vifaa vya shule kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Msinune iliyopo kata ya Msinune Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani leo Januari 11, 2021.
Mwanamitindo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Flaviana Matata, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete, viongozi wa Tarafa pamoja na viongozi wa Shule wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi waliopewa pedi za Lavy zinazotengezwa na kampuni ya Flaviana Matata leo Januari 11, 2021.

Mwanamitindo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Flaviana Matata, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete, viongozi wa Tarafa pamoja na viongozi wa Shule wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Msinune Mara baada ya kutoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi hao.
Mwanamitindo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Flaviana Matata akiserebuka na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Msinune.

TAASISI  ya Mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata  imetoa vifaa vya masomo ikiwemo mabegi pamoja na kalamu kwa  wanafunzi wa Shule ya Msingi  Msinune iliyopo  Msata  Katika Wilaya ya Chalinze  Mkoani Pwani.


Mkurugenzi huyo ambaye aligawa vifaa hivyo  kwa wanafunzi   wapatao  345   akisindikizwa  na Mbunge  wa Chalinze  Mheshimiwa  Ridhiwani  Kikwete.

Akizungumza  kabla ya kukabidhi  vifaa hivyo Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata Foundation alisema kuwa  , taasisi hiyo ilianza  kufanya  ukaarabati katika Shule hiyo mwaka 2016 huku akisema kwamba akilinganisha hali ilivyokua  awali na sasa ni tofauti kwani  Majengo yalikua chakavu tofauti na sasa ambapo wameweza kufanya ukarabati  , kuweka miundombinu ya  maji na umeme..

Aidha  Matata aliongeza  kwa kusema kuwa  Taasisi hiyo baada ya kumaliza  kukarabati majengo  hali  ambayo imeweka mazingira  rafiki  kwa wanafunzi, hivi sasa wanajipanga kujenga nyumba   za waalimu  huku akimuomba Mbunge wa Chalinze kusaidia baadhi ya vifaa vya  ujenzi ili kwa pamoja waweze kulifanikisha lengo hilo.

Akizungumza  kwenye mkutano huo Mbunge wa  Jimbo la Chalinze Ridhiwani  Kikwete alisema kuwa amepokea kwa mikono miwili ombi la  ujenzi wa  nyymba za Waalimu kwani  katika taasisi zetu  bado tunachangamoto   nyingi lakini kwa  kupitia Taasisi ya Flaviana Matata Foundation nina imani wote  kwa pamoja tutaunganisha nguvu kwa kutumia mfuko  wa Jimbo nyumba hizo za Waalimu tutazijenga.

"Flaviana umetupiga  teke  kutoka mbali kwani ukirudi miaka 20 nyuma wakazi wa Kijiji hiki cha Msinune hawakuwa na mwamko wa elimu tofauti na ilivyo sasa nakiri hilo" alisema  Kikwete huyo.

Alisema kuwa ana anamuomba Mwanamitimdo huyo wa Kimataifa kuwatatulia changamoto ya soko la  zao la Mananasi ambapo kwa kupitia Taasisi yako  unayo nafasi ya  ya kutusaidia  karika  kututafutia fursa  za soko la mananasi nje ya nchi  ikiwa ni katika kukuza uchumi wa Chalinze.

Kila inapofika mwanzo wa Muhula Taasisi ya Flaviana Matata hupeleka vifaa vya shuleni ,pia kwa kupitia Taasisi hiyo  wamekuwa  wakitoa udhamini kwa wanafunzi katika   Shule za Sekondari na Vyuo Vikuu nchini.

Wakati huohuo Flaviana Matata ametoa wito kwa wazazi kuacha kuwakatisha   watoto wao wa kike masomo na kukimbilia kuwacheza ngoma.

"Baba zangu na  mama zangu nawaomba sana  muachane na tabia ya kuwakatisha masomo  mabinti zenu kwani elimu ndiyo ufunguo  wa maisha  hivyo wakati  umefika sasa wa kuachana na  mila potofu ambazo zinapoteza matumaini ya njozi zao katika  maisha  yao  ya baadaye wao wakiweza  kusoma watakuja kuwa msaada mkubwa sana kwenu na kwa jamii nzima kwa ujumla.


Share To:

Post A Comment: