Saturday, 2 January 2021

KIZIMBANI WALIOHUJUMU MIUNDOMBINU YA BARABARA MANISPAA YA MOSHI WAFIKISHWA MAHAKAMANI,MEYA ATOA ZAWADI YA MILIONI 1

 Ni Takribani Wiki Mbili sasa tangu Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Moshi Juma Raibu atangaze kuwasaka kwa udi na uvumba watu wanaojihusisha na wizi wa taa Za barabarani katika Manispaa ya Moshi,hatimae leo Watuhumiwa 6 wamepandishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya Kula njama ya kutenda uhalifu na Kuhujumu Uchumi.


Akizungumza Nje ya Mahakama Mstahiki Meya Juma Raibu amesema Wizi na Uharibifu huo umeisababishia serikali hasara ya Milioni 59 na Madhara ya watu kuporwa na kukabwa katika maeneo mbalimbali kutokana na ukosefu wa Taa katika maeneo hayo.


Mstahiki Meya Juma Raibu amesema,nanukuu "Tunajua wako baadhi ya watu wana nia ovu na serikali ya awamu ya tano,wako watu wana nia ovu ya kukwamisha maendeleo,watu wanaiba miundombinu ya  barabarani kwajili ya kwenda kuuza,niwaambie katika awamu hii watakwama wao,Niwaombe sana wananchi wa Manispaa ya moshi kwanza mwamini  Maendeleo yote haya.

No comments:

Post a Comment