Friday, 1 January 2021

10 WASHIKILIWA KWA TUHUMA MBALIMBAI IKIWEMO WIZI, UHAMIAJI HARAMU NA MADAWA YA KULEVYA.NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


Watu kumi wanashikiliwa na jeshi la Polisi mkoa Arusha kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo wizi,uhamiaji haramu pamoja na madawa ya kulevya aina ya bangi.Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Salum Hamduni alisema kuwa mnamo tarehe Desemba 30,2020 saa nne asubuhi katika eneo la Olnjavitian kata ya Sombetini Halmashauri ya jiji la Arusha  jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata Ibrahim Ezekiel mkazi wa Mianzini akiwa na vitu mbalimbali vya wizi pamoja na vifaa vya uvunjaji.Kamanda Hamduni alieleza kuwa mtuhumiwa mwingine wa wizi akikamatwa Desemba 29,2020 saa mbili usiku maeneo ya Uswahilini katika Kata hiyo ni Zuberi Juma ambapo badhi ya vifaa hivyo ni pamoja na  TV,Laptop, Tablet ,Compressor, pasi, dryer, radio, spika, ving'amuzi,Subwoofer pamoja na vitu vingine vingi.Alisema kuwa tukio lingine ni la kukamatwa kwa wahamiaji haramu wanne pamoja na gari ambapo Desemba 30,2020 saa 5 usiku maeneo ya Ngaramtoni ya chini  askari wakiwa katika doria walifanikiwa kukamata gari aina ya Volvo lenye namba za usajili ZA 5043 na tela lenye namba za usajili TO 6713 zote za Malawi likiwa limebeba wahamiaji haramu nne raia wa Ethiopia ambao wameingia nchini bila kibali.


Alisema kuwa wahamiaji hao walikamatwa ni Tamerat Tagann,Mulukne Dasta, Adan Mamad, pamoja na Elias Zeleka amapo jeshi polisi linaendelea kuwashikilia  kwa hatua zaidi za kisheria ikiwa ni pamoja na kumtafuta dereva wa gari hilo ambaye alitelekeza gari na kukimbia.


Alifafanua kuwa tukio lingine ni la kukamatwa kwa watuhumiwa  wanne wakiwa na bangi ambao walikamatwa na  katika msako  Disemba 30,2020 saa 6:30 katika kijiji cha Olkokola Kata ya Lemanyata  wilaya ya Arumeru  jeshi hilo lilifanikiwa kumkamkamata Neema Eduward akiwa na mifuko miwili ya salfet yenye madawa ya kulevya aina ya bangi.Katika msako huo pia walifanikiwa kumkamata Lengimoo Sarayani akiwa na bangi kwenye mifuko ya salfet nyumbani kwake,Nashibai Musoyoki akiwa na bangi na misokoto katika mifuko pamoja na na Sendui Nyangusi akiwa na bangi kwenye mifuko mitatu ya salfet ambapo watuhumiwa wote wanashikiliwa na baada ya upelelezi kukamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwaajili ya kutolea uamuzi wa kisheria.


Aidha katika kuelekea mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya kamanda Hamduni alisema kuwa jeshi hilo limejipanga vyema kuhakikisha sikukuu hiyo inasherekewa kwa amani na utulivu ambapo pia imepiga marufuku makongamani au mikutano ya mkesha siku ya tarehe 31katika maeneo ya wazi nyakati za usiku kutokana na changamoto za kiusalama na badala yake ibada hizo zifanyike kwenye nyumba za ibada na mwisho ni saa 6:30 usiku. 


Pia alifafanua kuwa ni marufuku kuchoma matairi barabarani, kupeleka watoto disco toto, madereva kuendesha magari wakiwa wamelewa, magari ya abiri kutojaza abiria kupita kiasi pamoja na upigaji wa fataki kwa ambao hawatakuwa na vibali.

No comments:

Post a Comment