Mhandisi Joseph Richard Kimako,kutoka Mamlaka ya Elimu na ufundi stadi VETA,amewasilisha namna hasara na  upotevu unaopatika kabla na baada ya kuvuna katika zao la nyanya katika Mkutano wa 12 wa Kimataifa wa Taasisi ya wahandisi nchini uliofanyika Ngurudoto Arusha


"Zao la nyanya ni moja kati ya zao muhimu linaloimarisha afya ya mlaji lakini pia kipato kwa wazalisha wadogo hapa nchini" Eng.Joseph Kimako,kutoka mamlaka ya Elimu na ufundi Stadi VETA


"Tafiti yetu ilijikita katika Mkoa wa Morogoro katika wilaya ya Kilosa na Mvomero,katika Maeneo ya Doma na Dumila kwa wakulima wa Nyanya"Eng.Joseph Kimako,kutoka mamlaka ya Elimu na ufundi Stadi VETA


"Kuna upotevu Mkubwa wa nyanya kabla na baada ya kuvuna unaosababishwa na wakulima wetu kutopata Elimu Sahihi ya zao la nyanya"Eng.Joseph Kimako,kutoka mamlaka ya Elimu na ufundi Stadi VETA


" Kuna umuhimu mkubwa sana katika maeneo ya uzalishaji wa nyanya kujengwa viwanda vya usindikaji ili kuondoa hasara ya upotevu wa nyanya"Eng.Joseph Kimako,kutoka mamlaka ya Elimu na ufundi Stadi VETA


"Tunashauri pia kalenda za mazao za kilimo zifike kwa wakulima ili wakulima  walime zao hili kulingana na msimu mzuri wa soko la nyanya"Eng.Kimako,kutoka mamlaka ya Elimu na ufundi Stadi VETA


" Sisi kama VETA tutaendelea kuwasaidia wakulima kwa kuwashauri namna bora ya kupunguza hasara ya upotevu wa zao za nyanya kabla na baada ya kuvunwa"Eng.Joseph Kimako,kutoka mamlaka ya Elimu na ufundi Stadi VETA"

Share To:

msumbanews

Post A Comment: