Friday, 11 December 2020

MMOJA AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUCHOMA MOTO GARI MBEYA

 

E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz

              tanpol.mbeya@gmail.com

                                                                                                                             11 Desemba, 2020

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA KUCHOMA MOTO GARI.

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kumkamata SAM PHILIMON LIKWELILE [29] Mkata Ushuru wa Mazao na Mkazi wa Gombe Jijini Mbeya kwa tuhuma za kosa la kuchoma moto Gari yenye namba za usajili T.281 CZP Toyota IST mali ya SALOME SAMSON [31] Mhasibu RAPHAEL GROUP na Mkazi wa Majengo Mapya.

Ni kwamba mnamo tarehe 08.12.2020 majira ya saa 02:30 usiku huko Mtaa wa Majengo Mapya, Kata ya Nsalaga, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, Mtuhumiwa SAM PHILIMON LIKWELILE [29] alivunja kioo cha Gari namba T.281 CZP Toyota IST mali ya SALOME SAMSON [31] na kisha kuchoma moto sehemu ya ndani ya Gari hilo na kusababisha kuharibika na kisha kutoweka.

Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako na mnamo tarehe 10.12.2020 majira ya saa 18:30 jioni huko Mtaa wa Gombe, Kata ya Itezi, Tarafa ya Sisimba, Jiji la Mbeya na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa SAM PHILIMON LIKWELILE [29].

Katika mahojiano yaliyofanyika mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.


KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia RHODA SOMORA [66] Mkazi wa Itezi Jijini Mbeya akiwa na pombe haramu ya moshi [Gongo] lita 25.

Mtuhumiwa alikamatwa tarehe 10.12.2020 majira ya saa 21:00 usiku huko Mtaa wa Mwasote uliopo Kata ya Itezi, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya katika misako inayoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo. Atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Imetolewa na;

[ULRICH O. MATEI -SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

No comments:

Post a Comment