Na Mwandishi wetu.


Mbunge Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameendelea na ziara ya Kata kwa Kata ambapo ametembelea Kata ya Mkange Vijiji vya Matipwili, kitongoji cha Saadan Chumvi, Saadan kijijini na Kijiji cha Mkange akishukuru na kupokea kero za Wananchi.


Akiwasikiliza wananchi katika vijiji hivyo, wananchi hao walimweleza Mbunge changamoto nyingi zikiwemo za mipaka inayozunguka Hifadhi ya Taifa ya Saadan na Vijiji vya kata hiyo, Mheshimiwa Mbunge aliwakumbusha wananchi ahadi aliyoitoa Mheshimiwa Rais kipindi cha kampeni na sasa utekelezaji wa ahadi hiyo umeanza. Hivyo mbunge alitumia nafasi hiyo kuwaondoa wasiwasi wananchi hao.


Aidha, akiwaondoa hofu Wananchi hao Mbunge Ridhiwani aliwakumbusha kuwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anavifahamu vijiji vinavyozungumza hifadhi na  alishataja baadhi ya Vijiji vilivyo kwenye hifadhi ambavyo vitarasimishwa kwa Wananchi wakati alipokuwa Msata kwenye Kampeni hivyo kwa sasa watulie tusubiri Serikali yao itoe majibu. 


"Rais Dkt. Magufuli alivitaja baadhi ya vijiji ambavyo vipo pembezoni mwa hifadhi ambapo alivitaja vijiji hivyo kwa majina ikiwemo vya Matipwili, Saadan,Gongo, Mandamazingara. Pamoja na kuvitaja vijiji  hivyo niwa hakikiahie kuwa mimi niwahakikishie kuwa Namuamini Rais Magufuli na hili litatendeka kaka yalivyofanikishwa mengine mengi." Alieleza Mbunge Ridhiwani Kikwete.


Katika hatua nyingine Akijibu hoja ya kero hizo pia,  Mhe. Mbunge Ridhiwani Kikwete aliwataka Viongozi wa Vijiji na Vitongoji kukaa na Wananchi ilikujadili masuala muhim ya kushughulikia kero hizo ambazo zingine zinaweza kutatuliwa na viongozi hao.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: