Monday, 23 November 2020

TULIA ACKSON AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOIENDELEZA MBEYA MJINIMbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dr. Tulia Ackson amezungumza na Waandishi wa Habari nyumbani kwake na kuwaeleza ratiba yake kuwaona na kusikiliza hoja na kero za Wananchi ambapo amesema ratiba hiyo itakuwa mara mbili kwa kila wiki ikiwa ni siku ya Alhamis pamoja na Jumamosi.


“Tutakuwa na utaratibu wa kusikiliza Wananchi na kwa sababu Jimbo hili la Mbeya mjini ni kubwa na lina kata 36 kwahiyo tutakuwa na siku mbili kwa wiki kwa ajili ya kuwasikiliza Wananchi na tutakuwa na maeneo mawili tofauti, kwanza tutawasikiliza Wananchi katika eneo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na siku itakuwa ni Alhamis na muda ni kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni”-Dr. Tulia Ackson


“Upande wa Bonde la Uyole wao watasikilizwa siku ya Jumamosi ambapo eneo litakuwa ni katika ofisi za Tulia Trust zilizopo Uyole na zoezi hili linaanza wiki hii, nimeona nifanye hivyo kwasababu wakati mwingine Wananchi wamekuwa wakihangaika kumtafuta muwakilishi wao sasa nimeona mapema kabisa nitangaze utaratibu huo ili kazi iendelee”-Dr. Tulia Ackson


“Utaratibu utakuwa kwamba Mbunge anapokuwa Jimboni hizo kero na hoja zote atakuwa akizisikiliza mwenyewe na hata kama hatokuwepo basi wapo wasaidizi ambao watakuwa wakiwasikiliza Wananchi ikiwemo kero, changamoto pamoja na mawazo yao ambayo kwa pamoja yatasaidia kuhakikisha Jiji letu la Mbeya linasonga mbele kwa maana hiyo hata kama itatokea muda ambao sipo Jimboni basi wafahamu kwamba bado ofisi zitaendelea kuwa wazi kwa ajili yao”-Dr. Tulia Ackson

No comments:

Post a Comment