Na Geofrey Stephen  Arusha


Mbunge Mteule wa jimbo la Tarime mjini Mkoani Mara,Michael Mwita, amesema atapeleka muswada binafsi katika bunge lijalo la Jamhuri ya muungano Tanzania  ili kuondoa SHERIA inayoruhusu mtaala wa Elimu kubadilishwa muda wowote .


Akiongea katika Mahafali ya 7 ya kuhitimu Elimu ya  darasa saba katika Shule ya msingi Ghati Memorial yenye mchepuo wa kiingereza iliyopo Kata ya Terat, jijini Arusha,ambapo wanafunzi wapatao 145 walihitimu Elimu ya darasa la saba na kutunukiwa vyeti.


Mwita ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shule za Ghati Memorial,Nyahiri na Mlimani hapa Nchini ,amesema atahakikisha anawashawishi wabunge wenzake ili kupitisha muswada huo ambao anaamini ukifanyiwa marekebisho utakuwa mkombozi mkubwa katika sekta hiyo hususani  kwa wahitibu .


Alisema hatua ya Serikali kubadili mtaala wa Elimu Mara kwa Mara kunasababisha usumbufu kwa shule na wanafunzi pia hatua ya ufaulu inapungua


"Mtaala wa Elimu uliopo kwa sasa haukidhi mahitaji ya Mhitimu tunachotaka uboreshwe  ili kumjengea  Mazingira bora mhitibu aweze kukabiliana na soko la ajira  " alisema Mwita


Awali Mwalimu mkuu wa Shule hiyo ,Ndaro Nyahuga alisema kuwa jumla ya wanafunzi wapatao 145 walioanza darasa la kwanza wote  wamehitimu Elimu ya msingi shuleni hapo  na anaimani wote watafaulu vizuri kutokana na historia  ya Shule hiyo kufaulisha wanafunzi wote  kila mwaka.


Katika hatua nyingine Mwalimu mkuu alisema Shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya ubovu wa miundo mbinu ya barabara inayopelekea wanafunzi kuchelewa kufika shuleni , jambo ambalo  ameiomba Serikali kuzifanyia matengenezo barabara zote zilizopo jirani na Shule hiyo ili ziweze kupitika nyakati zote ikiwemo msimu wa mvua.


Kwa upande wa wahitimu  kupitia risala yao iliyosomwa na Zara Suleiman waliishukutu Shule hiyo kwa kuwapatia Elimu iliyo bora ila waliwaomba Wazazi kusaidia malezi kwa watoto wao na kuepuka kuwaachia walimu kwani baadhi ya wanafunzi wenzao wanatabia ya utoro inayosababishwa na ufuatiliaji hafifu wa Wazazi.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: