_MG_9996



MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro wamesema kwamba watatumia mashindano ya Shimuta yanayofanyika Jijini Tanga kama sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani. 

Hayo yalisemwa na Kiongozi wa michezo wa Mamlaka hiyo na Mjumbe wa kamati tendaji ya Shimuta, Marcel Kitulo mjini hapa ambapo alisema wamekuja kushiriki wakiwa wamebeba ujumbe wao shughuli zao ni za utalii. 

Alisema hivyo watahamasisha pia kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Mapango ya Amboni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ikiwemo kuwaeleza mazuri ya ngorongoro. 

“Tutatumia mashindano hayo ya Shimuta kama sehemu ya kuhamasisha wafanyakazi kufanya utalii wa ndani kutembelea vuvutio vyetu ikiwemo Mapango ya Amboni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro”Alisema 

Aidha alisema kwamba mashindano hayo yamekuwa yanakua kutokana na timu kuongezeka kila mwaka na hivyo kuongeza mwamko na ushindani pia 

Hata hivyo alisema kwamba wao wamefika kushiriki lakini pia kama wadhamini wa mashindano hayo kutokana na kusaidia baadhi ya mahitaji muhimu shimuta na wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara. 

Alisema pia wao wanashiriki kujenga afya za wafanyakazi kwa sababu mashindano hayo ni zaidi ya michezo ya uwanjani yanatoa fursa wafanyakazi kutengeneza mtandao kwa wafanyakazi wa umma na makampuni binafsi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: