Na Vumilia Kondo


Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa wamefanikiwa kuandaa mpango wa matumizi Bora ya aridhi kwa kushirikiana na Shirika la kuhifadhi misitu ya asili nchini Tanzania (TFCG)SHIRIKA la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG)na wadau wake .



Pamoja na hayo Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo imetoa ombi kwa TFCG pamoja na wadau wake waendelee kuiwezesha halmashauri hiyo katika suala la uhifadhi wa misitu ya vijiji kwa kuitenga na kuhuwisha mipango ya usimamizi shirikishi ya vijiji iliyopitwana wakati.


Hayo yameelezwa  na Mratibu wa Mradi wa Kuhifadhi Misitu kwa Kuwezesha Biashara ya Mazao ya Misitu Tanzania(CoforEST)Aigen Mwilafi ambaye pia ni Ofisa Misitu Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.




Aidha amesema kuna takribani misitu 11 haijatengwa kuwa misitu ya hifadhi ya vijiji na kuna mipango ya usimamizi shirikishi wa misitu ya vijiji 45 imepitwa na wakati inahitaji kuhuhishwa.


"Tunaomba muendelee kushirkiana nasi katika kutekeleza hayo."


Kwa upande wake muwakilishi wa Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Peter Selder amesema Ubalozi wa Uswisi nchini kupitia Shirika lake la maendeleo wapo Tayari kuendelea ushirikiano katika kuhifadhi shirikishi wa misitu Ili kupitia Tanzania kwenye nchi zinazoongoza kwa uharibifu wa misitu.

"Nimefurahi kuona namna jamii inavyoshiriki na kunufaika moja kwa moja na hii itasaidia sana kwani wanapata motisha ya moja kwa moja kwao binafsi na vijiji na hii inawafanya waone umuhimu wa kuitunza na kuilinda kwa ajili ya vizazi hivi na vizazi vijavyo, alisisitiza.



Kwa upande wa Mkurugenzi wa MJUMITA, Rahima Njaidi amesema TFCG na MJUMITA wamedhamiria kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya misitu na mazingira nchini na wanaamini kwa ushirikiano uliopo kati yao na wadau wengine wakiwemo wananchi wa maeneo ambayo miradi inatekekelezwa mafanikio makubwa yatapatikana na kuleta tija kwa umma.


Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mahenge wilayani Kilolo Said Halfan Muhina amesema wameomba msaada wa kupatiwa mafunzo zaidi ambapo amefafanua licha ya kuelimishwa bado wanaomba waendelee kupatiwa elimu zaidi na kwamba wanamini kile ambacho kitapatikana kitasaidia kuleta maendeleo ya kijiji chao.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: