Mchakamchaka wa kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia CCM Dr. Tulia Ackson, umeendelea tena leo October 17, 2020 na safari hii ilikuwa ni zamu ya kata ya Kalobe Jijini humo ambapo amewaeleza baadhi ya mambo makubwa yatakayonufaika nayo Wananchi wa Jimbo hilo endapo watakipigia kura za ndio chama chake kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 28, 2020.


 “Hapa Kalobe nafahamu kuna changamoto nyingi, zipo baadhi ambazo zimepunguzwa ila nyingi zilikwama kwasababu mlikosa Mbunge mwenye connection ya kuweza kuzitatua changamoto zenu na safari hii nimekuja kwenu Tulia ninayeweza kutulia Bungeni na kuwasemea matatizo yenu”- Dr. Tulia Ackson


“Nafahamu wazi mshashazisikia habari zangu ni ni yapi nimeyafanya hapa Mbeya Jiji ikiwemo hapa Kalobe, sio kwenye afya, elimu, miundombinu n.k na yote hayo nimeyafanya nikiwa sio Mbunge wenu lakini niliyafanya kwa mapenzi ya dhati kwa Wananchi wa Mbeya. Safari hii chagueni Tulia na Magufuli muone balaa lake hapa”- Dr. Tulia Ackson


“Najua mtataka walau kusikia kwa uchache mimi Tulia nimewafanyia yapi hapa Kalobe, tukianza na hapo Shule ya Sekondari Kalobe mimi Mbunge wenu wa kujiongeza nilishapeleka Computer tano na printer ambapo ni zaidi ya Tsh: 10,750,000/- nab ado tunazo changamoto zao nyingi tutazitatua zote, lakini kwa ujumla hapa Mbeya mjini kwenye sekta ya Elimu mimi Mbunge nimeshatoa zaidi ya shilingi milioni mia mbili  (Tsh: 200,000,000/-) na hapo sina mfuko wa Jimbo lawa kitu gani labda ndio maana sijanenepa kwa sababu ya kuwatumikia wana-Mbeya”- Dr. Tulia Ackson


“Ndugu zangu mtu anapokuja kwenu kuwaomba kura muulizeni kwanza umetufanyia nini kabla hujaja hapa? Mbeya Mjini hatudanganyiki tena na safari hii tunaenda na Tulia na Magufuli kwa ajili ya maendeleo yetu na wala hatutaki propaganda zilizoganda. Maendeleo ya kweli yanatoka CCM pekee na wala sio kwingineko”-Dr. Tulia Ackson

Share To:

msumbanews

Post A Comment: