NA  MWANDISHI WETU.

KAMPUNI ya TMS Consultants Ltd, inayojishughulisha na ushauri wa biashara na uwekezaji nchini inatarajia kukutana na Vijana zaidi ya 200 wa Vyuo vikuu ilikuwapatia mafunzo ya kidigitali kwa ajili ya kupunguza tatizo la ajira.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TMS Consultants, Sebastian Kingu ametoa wito kwa Vijana mbalimbali walio Vyuoni haswa wanafunzi wa Shahada ya Kwanza waliomaliza mwaka wa kwanza na sasa wanasubiri kuingia mwaka wa Pili, Novemba 2020 kuhamasika na kujitokeza kwa wingi kwenye tukio hilo litakalofanyika Oktoba 3 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

"Programu hii kwa Tanzania ndio inakuwa ya kwanza kufanyika na sisi TMS Consultants tunakuwa kampuni ya kwanza kuanzisha.

Ambayo kitaalamu inajulikana: 'Digital Online Mentorship Internship Training  for Employment Creation Programme' ambapo vijana hao wa Vyuoni wataweza kupatiwa elimu na namna kukabiriana na changamoto za ajira.

Sebastian Kingu aliongeza kuwa, katika uzinduzi huo hiyo Jumamosi ya Oktoba 3, hakutakuwa na kiingilio na walengwa wote wanakaribishwa tukio litakalofanyika katika kumbi za Peacock Hotel jirani na Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

"Lengo kufikia wanafunzi wengi zaidi. Kwa sasa tunatarajia kuwa na wanafunzi 200. Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea tovuti yetu ya www.tmsconsultants.co.tz ambayo taarifa mbalimbali kuhusiana na programu hii na kushiriki" Alisema Sebastian Kingu.

Sebastian Kingu aliongeza kuwa, baada ya uzinduzi huo pia watafanya uzinduzi mwingine kwa  washiriki kutoka mikoani.

"Oktoba 10 mwaka huu pia tutakuwa na uzinduzi mwingine na walengwa ni walewale wa Shahada ya kwanza ambao hawakushiriki uzinduzi wa awali utakaofanyika Oktoba 3." Alisema Sebastian Kingu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TMS Consultants, Asajile Mwichande alisema lengo ya programu hiyo ni kupunguza suala la ukosefu wa ajira haswa kwa vijana wanaotoka Vyuoni.

"TMS Consultants Ltd kupitia programu hii kwa Vijana wetu wa Vyuoni itakuwa chachu ya kukabiriana na changamoto ya ajira wakiwa wanaendelea na masomo"  alisema Asajile Mwichande.

Programu hiyo ni muhimu kwa Tanzania inaenda kuwa ya kwanza  hivyo walengwa wameombwa kujitokeza kwa wingi kutoka Vyuo mbalimbali.

Mwisho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: