Saturday, 12 September 2020

USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA TEKNOLOJIA ILIYOBORESHWA ITASAIDIA KUTATUA CHANNGAMOTO ZAO


Na Namnyak Kivuyo, Arusha.

Ushiririki wa wanawake katika utengenezaji na uboreshaji wa  teknolojia ni muhumu  kwani utawezesha  teknolojia hizo kukudhi mahitaji yao pamoja na kutumika katika jamii na kuwa endelevu.

Hayo yameelezwa na mhadhiri wa masomo ya teknolojia  (ICT) kutoka chuo kikuu cha  Mzumbe Dr  Tupokigwe Isayah wakati akiwasilisha mada katika semina iliyotolewa na shule ya wanawake Arusha ya utawala wa mtandao(ARUSHA WOMEN SCHOOL OF INTERNET GOVENENCE) kwa wanawake kutoka asasi mbalimbali za kiraia ,walemavu, wanasheria pamoja na waandishi wa habari.

Dr Tupokigwe alisema kuwa ni muda sahihi wa ushiriki huo wa wanawake kwa kutoa maoni  na kuelewa teknolojia ambapo kwa kufanya hivyo kuwa na uhakika wa teknolojia iliyoboreshwa na inayotumika katika jamii kwa maedeleo endelevu ambapo pamoja na kuhakikisha kuwa teknolojia inakidhi mahitaji yao lakini pia itasaidia kuleta matumizi ya vifaa mbalimbali vya teknolojia ambazo zimetelekezwa mitaani kutokana na kutokujua matumizi sahihi.

Alieleza kuwa kama wanawake wamekuwa watumiaji wa teknolojia iliyoboresha wanatakiwa kuangalia na kujaribu kuelewa mchakato mzima kwanzia kifaa kinapoanza kufanya kazi, hatua zilizotumika, changamoto walizopitia pamoja na vitu vyote wanavyoviona vitakavyo wafanya washindwe kutumia taknolojia husika.

"Wengine wanaweza kusema kwamba hawajui teknolojiainaendaje na hawajui vifaa vyake vikoje, na wasishiriki kwa njia yoyote kupanga au kutoa mapendekezo ya jinsi mfumo utakavyokuwa au katika kuendeleza lakini mwisho wa siku wanahitaji utumia kifaa lazimz utakutana na changamoto ya kutumia teknolojia ambayo sio rafiki kwao" Alisema DrTupokigwe.

Alifafanua kuna dhana kuwa sehemu ya kutengeneza teknolojia nijukumu la watu wachahe lakini kihualisia ni hatua ambayo kila mtu anatakiwa kuchukua kwani ushiriki huo mwisho wa siku waandaaji wanaweza kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kuendelea teknolojia hizo ili ziweze kukidhi mahitaji ya watu mbalimbali hivyo watu wanatakiwa kuwepo katika kutengeneza.

"Alisisitiza kuwa baada ya kuona vitu vinavyowafanya washindwe kutumia teknolojia hizo  au kuona mambo yanayoweza kuwaingiza katika hatari wasikae kimya bali watoe maoni yao na kutuma kwa wahusika wa teknolojia hiyo na baada ya hapo watengenezaji hao wataweza ukaa chini na kuamua ni jini gani wanaweza kurekebisha.

 Esther Mengi mwanzilishi wa kampuni ya Serensic  Afrika inayojishulisha na masuala usalama wa kwenye mtandao alisema  ili kuhakikisha usalama wako mtandaoni upotuma ujumbe wowote na kupokea majibu kabla ya kufanya  jambo lolote unapaswa kuhakikisha ujumbe huo umetoka kwa muhusika na haina kitu chochote cha tofauti.

"Nimefurahi kuona wanawake wengi katika mfumowa teknolojia wanafanya wanafanya mambo makubwa na yatofauti na semina hii imetupa nafasi ya kuelezana  changamoto zinazowakabili wanawake katika teknolojia na tumeweza kujua ni kwanini mtu awe salama akiwa mtandaoni" alieleza.

Alieleza  kuwa ni lazima mtu alinde taarifa zake kasababu mtu anaweza kutumia taarifa hizo zilizopo katik mitandao ya kijamii na kutengeneza akaunti feki na kuanza kuitumia kama wewe kufanya uhalifu wa aina yoyote ikiwemo kutapeli, kupotosha jamii  na mambo mengine aliendelea kusema kuwamtu asipoweka nywila imara{passoword} katika akaunti zake  kwenye mitandao mtu mwingine anaweza kuingi na kujibu au kutuma ujumbe  kwa watu wao wa muhimu na wakati mwingine hata kuwaharibia kazi .

Aidha alieleza kuwa usalama wa mtandao hasa wakati huu vyama vinapofanya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 28 mwaka huu  ni muhumu kwani kipindi hiki wameon mifumo mingi ikidukuliwa kutokana na kunaona watu wamekuwa wakifuatilia kinachoendelea na wahalifu hao wanatumia nafasi hii kufanya uhalifua wa kimtandao hivyo wawe makini.

"Hasa katika kipindi hiki usiwe mwepesi wa kusambaza taarifa yoyote unayoipokea kabla ya kuhakikisha  je taarifa hiyoni ya kwli na chanzo chake ni sahihi  na wakati mwingine ujiulize je kuna umuhimu wa kusambaza kwasababu taarifa zingine zinaweza kuwa za uongo na unaposambaza zinaweza kuleta machafuko" alisema Bi Mengi.

Sambamba na hayo  pia alizungumzia changamoto  walemavu wa kuona{vipofu } katika teknolojia zilizopo katika tasisi za fedha ambapo  alisema uwa walemavu hao wanapoenda kutoa fedha ni lazima waende na msaidizi kutoka na mifumo iliyopo utokuwa rafiki ikiwa ni pamoja na baada ya kutoa fedha ujumbe kuingia katika simu zao kwa nja ya maandishi badala ya sauti hivyo taasisi hizo wana wajibu wa kuboresha teknolojia ili walemavu waeze kupata  huduma kwa urahisi  na haraka.

Linda Malisa mwalimuwa watoto wenye ulemavu kutoka shule ya msingi Ilboru ambaye allikuwa ni mtafsiri wa Lugha za alama katika semina hiyo alisema kuwa matumizi ya mtandao yamewarahisishia walemavu  kuwasiliana japo kuna badhi ya vifaa bado sio rafiki hasa kwa alemavu wa kuona[vipofu} kutokana na kutokuwa kwa maneno na namba za nukta nundu katika taasisi zao pamoja na jumbe za sauti zitakazowawezesha kupata huduma ipasavyo.

"Taasisi hasa za fedha ziboreshe teknolojia zao wa kuweka jumbe za sauti na matumizi ya nukta nundu ili walemavu a kuona waweze waweze kuwa salama wao pamoja na rasilimali zao" alisema Mwalimu Linda.

Naye Peter Mbando mmoja wa waandaji wa semina hiyo alisema kuwa dhumuni la kuelekeza mafunzohayo kwa wanawake ni uwasaidia katika kipindi cha digitali kuwapa elimu ya mtandao kwani dunia hivi sasa vitu vingi vinaendeshwa kwa njia ya mtandao .

"Mafunzo haya ni kaajili ya kuwaezesha wanawake kuwa makini na mitandao kwani nchi nyingi hivi sasa zinahurika na habari za uongo ambazo zinaweza kuleta mtafaruku katika jamii ili kuondosha amaniiliyopo hivyo ili kulinda amani ya nchi tumewapa elimu na maarifa yatakayowasaidia kujikinga na uhalifu wa mtandaoni na kufuata sheria zilizowekwa " alieleza Peter Mbando.

Hata hivyo semina hiyo imeandaliwa na taasisi ya Kuza Africa na kituo cha kuaendeleza cha kuwaendeleza vijana na uongozi{CENTER FOR YOUTH EMPOWERMENT AND LEADESHIP} kwa udhamini wa Locolization Lab, Facebook, ICANN na AFRINIC

No comments:

Post a comment