Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Idd Kimanta, ameipongeza benki ya National Microfinance Bank (NMB) kwa kuanzisha huduma wenzeshi ya malipo ya kabla bila kuwa na akaunti kwa wakala utalii.

Ametoa pongezi hizo alipokutana na uongozi wa benki hiyo ofisini kwake,amewaeleza amefurahishwa na huduma hiyo kuletwa katika Mkoa wa Arusha ambapo ndipo kwenye kitovu cha utalii.

Amesema,huduma hiyo itasaidia sana katika kurahisisha malipo mbalimbali kwa watalii wenyewe na hata wakala wa utalii.

Akitoa maelezo ya jinsi huduma hiyo itakavyofanya kazi Afisa Mkuu wa wateja wakubwa bwana Alfred Shayo, amesema huduma hiyo itasaidia kuwapunguzia muda wa kufanya malipo kwa foleni kwa watalii na mawakala wa utalii.

Vile vile huduma hiyo itaongeza makusanyo ya kodi kwa serikali kwani kila malipo yatakuwa yanafanyika kwa mtandao na hivyo itapunguza wizi wa mapato ya serikali.

Bwana Shayo, amesema huduma hiyo itawasadia hata wafanyabiashara wa mitandaoni kwa kuwarahisishia manunuzi kwa kutumia kadi ya malipo kabla bila kuwa na akaunti na ina uwezo wa kubadili aina 15 za fedha za kigeni.

Kadi hiyo ya malipo ya kabla itawasaidia wateja kupunguziwa makato ya mara mara pindi wanapofanya miamala ya mbalimbali.

Amesema, kadi hiyo ya kieletroniki itawasaidia hata wakulima wanapofanya malipo yao mbalimbali.

NMB wamezindua huduma ya malipo kabla kwa kutumia kadi ya kieletroniki bila kuwa na akaunti mapema wiki hii jiji Dar es Salaam, mahususi kabisa katika kusaidia malipo mbalimbali hasa kwa wakala wa utalii.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: