Tuesday, 22 September 2020

PAULINA GEKUL: MAGUFULI HAJAWAHI KUWASAHAU WANANCHI.


Na John Walter-Babati

Mbunge anaesubiri kuapishwa baada ya kupita bila kupingwa Jimbo la Babati Mjini Paulina Gekul amesema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi chini ya  Rais John Pombe Magufuli haijawahi kuwasahau wananchi.

Ameyazungumza hayo leo Septemba 22,2020 kwenye kampeni za Kuomba kura za Chama cha Mapinduzi kwa Mbunge, Diwani na Rais, zilizofanyika katika Kijiji cha Nakwa na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)  Taifa, Kheri James.

Gekul amewaambia wananchi kuwa Wema waliofanyiwa na  Rais Magufuli katika Jimbo la Babati Mjini kwa kipindi cha miaka mitano, fadhila kubwa ni kumpigia kura pamoja na wabunge na maiwani ifikapo Oktoba 28,2020.

"Hakuna haja ya kukinyima kura chama cha Mapinduzi,tuna kila sababu ya kuipa kura Ccm tukamilishe yaliyobaki" alisema Gekul

Mbunge huyo amesema Kijiji cha Nakwa ni Kijiji cha faraja na  Mfano  katika maendeleo Jimbo la Babati Mjini  kwa kuwa kwa nguvu zao  wameweza kujenga shule ya Msingi na Sekondari ya Kisasa pamoja na ujenzi wa Zahanati.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Rais John Magufuli kijiji cha Nakwa kimepokea shilingi milioni 801 ambazo zimekamilisha Mradi wa maji ambao ulikwama kwa miaka Mingi na kwa sasa wananchi wanafurahia huduma ya maji.

Aidha amesema katika kunusuru wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shule, Serikali imesaidia kukamilika kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari Nakwa na kupata usajili kamili ambapo awali ilikuwa kama shule shikizi ya Bagara Sekondari.

Gekul amesema pamoja na hayo serikali ya Rais Magufuli imetoa shilingi Milioni 152 kwa ajili ya Ujenzi wa Mabweni ya watoto wa kike ambao unaendelea kwa sasa.

Kijiji cha Nakwa kilichopo kata ya Bagara, kina wapiga kura zaidi ya elfu tatu 3000.

No comments:

Post a comment