Friday, 18 September 2020

ILANI YA UCHAGUZI YA CHADEMA YA MWAKA 2020/2025 INA MAPUNGUFU MAKUBWAWilliam Peter Ndilla

Jana nilitumia Masaa angalau Manne ya kupitia kwa kina Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya Mwaka 2020/2025.

Mambo Mengi ambayo yameainishwa na Ilani hiyo ni Marudio ya Ilani ya CCM ya Mwaka 2015/2020 Kama eneo la elimu bure na Mengine Mengi.

Nikawa najaribu kuangalia Maeneo ambayo yana Upekee Katika Ilani ya Chadema nikakutana na Vitu ambavyo kwa hakika vinanipa wakati Mgumu Kujua Mantiki ya Ilani hiyo.

Ilani ya Uchaguzi Bora ya Chama Cha Siasa Kila Siku nasisitiza lazima iwe na Sifa kuu Tatu.

Moja ni lazima Ilani ya Uchaguzi ya Chama Makini iwe na Maono na Malengo Mapana lakini ambayo yanapimika"Realistic and Measureable".

Ni Ukweli kuwa Ilani ya Chadema inawezekana ina Maono Makubwa lakini Je ni kwa kiasi gani inapimika?Uhalisia ni Kitu Muhimu Sana kwa Ilani Yoyote Maana baada ya Miaka Mitano Ilani ya Uchaguzi Upimwa na Wapiga Kura.

Pili Ilani ya Uchaguzi lazima ianishe We itapata rasilimali fedha za Kutekeleza Ilani hiyo.Ilani ya Uchaguzi ya Chadema inatakiwa Iseme wapi itatoa Rasilimali fedha kwa ajili ya Kutekeleza Ilani na Mipango ya Kila Mwaka ya Kibajeti.

Kwa bahati Mbaya Ilani ya Uchaguzi ya Chadema Kila Ukurasa inajaribu Kufinya Wigo wa Kukufanya Kodi kwa kupunguza tozo Mbalimbali Kama ambavyo nitaenda kuainisha hapo baadae.

Tatu Ilani bora lazima iwe na Watu walio tayari Kutekeleza Ilani hiyo kupitia Mipango Mbalimbali  ya Serikali.

Sijajua kwa kiasi gani Serikali ya Chadema itaweza kuyasimamia haya kwa Uaminifu na kwa wakati.

Ilani ya Uchaguzi ya Chadema inajaribu kuainisha Maeneo ambayo itayapa Kipaumbele Kama itapewa ridhaa ya kushika dola au Serikali na hapo Ndio Mjadala wangu Unapoanzia.

ILANI YA CHADEMA INATOA AHADI YA KUONGEZA  MISHAHARA MINONO NA KUPANDISHA MADARAJA WAFANYAKAZI WOTE WA SERIKALI.

Ilani ya Uchaguzi ya Chadema ya 2020/2025 inasema inataka kuongeza Mishahara kwa Wafanyakazi wa Serikali na Kuwapandisha Madaraja Wafanyakazi.

Hii ina Maana Kuwa Serikali ya Chadema italazimika kuongeza Makusanyo ya Serikali mara dufu hili Kuwezesha Upatikanaji wa Fedha za kulipa Mishahara Pamoja na gharama za kupandisha Madaraja Wafanyakazi hao.

ILANI YA CHADEMA INASISITIZA KATIKA KUPUNGUZA VYANZO VYA MAPATO KUPITIA KUPUNGUZA KIASI CHA  KODI.

Wakati Ilani ya Uchaguzi ya Chadema Ukurasa wa 28(4.2.1) inajinadi Kuongeza Mishahara Minono kwa Wafanyakazi wakati huo huo inasema itajaribu Kupunguza Kodi Katika Maeneo haya.

Moja,Kupunguza Kiwango Cha Kodi ya Makampuni"Corporate Tax" Mpaka kufikia asilimia 15 itokanayo na faida.

Hii ina Maana kuwa Kama Chadema itapunguza Kodi ya Makampuni Matokeo yake yatakuwa kushuka kwa Makusanyo ya Serikali.

Unawezaje kupunguza wigo wa kodi wakati huo huo Ukaweza kuongeza Mishahara na kupandisha Madaraja Wafanyakazi wako?Hizi ni ahadi hewa kwa Wapiga Kura.

Ilani ya Chadema pia inalenga kupunguza Kodi ya Ongezeko la Dhamani"VAT" Mpaka kufikia asilimia 10.

Hii ina Maana Ilani ya Uchaguzi ya Chadema inaenda kupunguza Uwezo wa Serikali kukusanya Kodi hivyo lazima itakosa Uwezo wa kuhudumia Miradi ya Maji,Barabara na Kilimo Cha Umwagiliaji.

Ilani ya Uchaguzi ya  Chadema pia inalenga Kupunguza Kodi ya Ardhi kwenye Viwanja Vyenye Hati hivyo pia kwenda kupunguza Uwezo wa Serikali Kukusanya na Kuhudumia Miradi ya Maendeleo.

Ilani hi inakosa Uhalisia na kushindwa Kusema na kuainisha Vyanzo Vipya vya Mapato ya Serikali Kama ambavyo Serikali ya awamu ya tano inafanya.

Ilani ya Chadema ya Mwaka 2020/2025 inasema inataka kutoa elimu bure kuanzia Shule za awali Mpaka elimu ya Juu.

Mikopo ya elimu ya Juu Pekee yake kwa Mwaka kwa  Wanafunzi wa elimu ya Juu ni Zaidi ya Billion 250 fedha za Kitanzania na hapo bado gharama za Uendeshaji wa Elimu ya Sekondari na elimu ya Msingi.

Sasa Sijui fedha hizi zitatoka Wapi Kama Serikali ya Chadema inaota kupunguza Kodi kwa Kasi hii?

Serikali ya Chadema Kama itapata nafasi ya kushika dola inatarajia kutoa Mikopo kwa Wanafunzi Vyuo vya Ufundi Kama Veta na Vyuo vya Ualimu(Ukurasa 36) Ilani ya Chadema 2020/2025.

Serikali ya Chadema pia ina Mpango wa kupunguza Kodi Katika Mapato(PAYE) kwa Mpaka kufikia asilimia 8.

Mapato na fedha za kuweza kuhudumia Miradi na  Mikopo kwa Wanafunzi zitatoka wapi?Kuna tatizo Kubwa hapa kuhusu Utekelezaji wa  Ilani ya Chadema ya Mwaka 2020/2025.

Ilani ya Uchaguzi ya Chadema Ukurasa wa 48(h) inasema Serikali ya Chadema itapunguza Kodi kwa Taasisi za fedha ambazo zitakopesha Vijana wa Kitanzania kwa kuingia Mikataba ya Kisheria na Taasisi hizo hili kufanikisha hilo.

Hii ina Maana kuwa Serikali ya Chadema inaenda Kubana Wigo wa Makusanyo wa Serikali ya Chadema unazidi kubanwa na hivyo kukosa Sifa ya pili ya Ilani ya Bora ya Chama Cha Siasa ambayo ni Uwezo wa kuainisha Vyanzo vya fedha za Kutekeleza Ilani hiyo.

ILANI YA UCHAGUZI YA CHADEMA INA NDOTO NA  MAONO MAKUBWA HUKU IKIENDELEA KUSISITIZA UVUJAJI WA MAPATO YA SERIKALI HIYO.

Kwa hakika Ilani ya Chadema ya 2020/2025 ina Maono Makubwa lakini yanakosa Uhalisia kwa kushindwa kuainisha Vyanzo vya Mapato na kuongeza Wigo wa Mapato ya kuweza Kutekeleza Ilani na Mipango ya Kibajeti.

Ilani hii imeshindwa Kabisa kuonyesha Wapi itaenda Kupata fedha za kutosha za Kutekeleza Maono na Malengo Yao.

Lazima Watanzania na Wapiga Kura wa Tanzania tutumie Mda  mwingi kuzisoma Ilani ya Vyama Vyote na kuzipima kabla ya Kwenda kwenye Sanduku la Maamuzi la  Kupigia Kura.

Ilani ya Uchaguzi ya Chama ya  Kuombea Kura haipaswi kuwa na Malengo yasiyo na Uhalisia kwani Matokeo ya kufanya hivyo ni kupunguza Ushawishi wa Chama kwa Wapiga Kura Kutokana na kushindwa Kutimiza Matarajio ya Wapiga Kura" Failure to Meet Voters Expectations".

+255759929244
Tanzania Kwanza.
Uzalendo Kwanza.
Maendeleo Kwanza.

No comments:

Post a comment