Thursday, 20 August 2020

Ni Gekul tena kugombea Ubunge Babati mjini kwa tiketi ya Ccm.

Na John Walter-Manyara
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Babati mjini Mkoani Manyara Paulina Philipo Gekul  ameshinda kura za maoni  kutoka Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Gekul ametangazwa leo jijini Dodoma na Katibu wa Itikadi na uenezi Ccm, Ndugu Humphrey Polepole.

Awali Gekul kwenye mchakato wa kura za maoni katika jimbo hilo alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 61, ambapo aliekuwa mbunge wa viti maalum mkoani Manyara Ester Mahawe aliongoza kwa kura 91 akifuatiwa na Werema Chambiri aliepata kura 77 kutoka kwa wajumbe.

Awali Gekul alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kabla ya kukihama chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi ambapo aliendelea kuwa Mbunge kwa tiketi ya Ccm baada ya kupita bila kupingwa.

Uchaguzi Mkuu hapa nchini unatarajia kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020 ambapo wananchi watapata fursa ya  kuchagua Madiwani, wabunge na ngazi ya Urais.

No comments:

Post a Comment