Na Esther Macha,Mbeya

MSIMAMIZI wa Uchaguzi jimbo la Mbarali mkoa wa Mbeya, Kivuma Msangi amewataka Wagombea wa vyama mbalimbali vya Siasa kuwa chachu ya kuhimiza amani na utulivu katika kipindi chote cha kampeni.

Msangi ametoa kauli hiyo wakati akipokea na kudhibitisha fomu za mgombea Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi CCM jimbo la Mbarali Francis Mtega katika ofisi za tume ya uchaguzi.

Amesema kuwa yeye kama msimamizi wa uchaguzi hata furahishwa kuona wagimbea wanakuwa chanzo cha kuhamasisha vurugu na chuki zinazo weza kuwa chanzo cha kuvunja amani.

"Wagombea nawaomba sana, fanyeni kambeni za ustaarabu, zisizo gawa wananchi na kujenga chuki, kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kubwa kisheria, na mimi kama msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hili la Mbarali sitafurahishwa na jambo hilo" amesema Msangi.
Kwaupande wake mgombea Ubunge Jimbo la Mbarali  (CCM) Francis Mtega, amesema kuwa kwa kushirikiana na chama chake atahakikisha anasimamia kikamilifu amani na mshikamano katika kipindi choote cha kampeni.

"Nakishukuru sana chama changu kuniami kupeperu bendera, nitahakikisha nafuata maelekezo yote ninayopatiwa" amesema Mtega.

Katika zoezi hilo la urudishaji wa fomu, mgombea huyo ameambatana na viongozi wa chama, huku akisindikizwa na mamia ya wanachama  wa chama hicho.

*Mwisho*
Share To:

msumbanews

Post A Comment: