Tuesday, 2 June 2020

Wagombea CCM Stop kutumia matarumbeta, watakiwa kuchukua fomu kimya kimya


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, amesema kuwa wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao, hawapaswi kutumia matarumbeta wakati wanaenda kuchukua fomu za ugombea, badala yake waende kimya kimya na matarumbeta yatapigwa mara baada ya chama kumteua mgombea.

Polepole ameyabainisha hayo leo Juni 2, 2020, wakati wa uzinduzi wa kituo maalum cha wananchi kutoa taarifa za uchaguzi kimaadili ili kuwabaini wala na watoa Rushwa katika kipindi cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba, 2020.

"Mchakato utaanza baada ya kuwatangazia na ndiyo kwa unyenyekevu na siyo kwa mbwembwe, utakwenda taratibu na si kwa matarumbeta kwenye ofisi ya chama kupata fomu yako, ukiipata kaijaze kwa umakini na kuirejesha, tarumbeta zitakuja baada ya kupata mtu mmoja hodari atakayeiwakilisha CCM kwenye uchaguzi" amesema Polepole.

Aidha Polepole ametoa rai kwa wananchi kwamba, wasidanganyike na wale watu wanaopita katika maeneo yao kujitangaza kwamba wameagizwa na Mwenyekiti wa chama kugombea, kwa kuwa ni walaghai na wasiwasikilize kwani hakuna mtu aliyeagizwa kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment