Kwa miaka mingi kulijengeka utamaduni kwa viongozi wengi hapa nchini kutoa maagizo mbalimbali bila kufanya ufuatiliaji kitendo kilicholeta tabia ya uzembe kwa watendaji wa umma kutotekeleza maagizo hayo na hivyo kusababisha kutokamilika kwa miradi mingi na upotevu mkubwa wa fedha za umma.

Katika kipindi cha miaka mitano ya serikali ya awamu ya tano kimekuwa kipindi tofauti sana kwa upande wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwani Waziri Jafo amekuwa mwiba kwa wazembe Kwani kila kinacho agizwa kinafuatiliwa hatua kwa hatua.

Katika ziara yake ya leo Mkoani Songwe tumeshuhudia miradi iliyotolewa maelekezo miezi michache ikifuatiliwa mmoja baada ya mwingine.

Faraja kubwa imekuja kwa viongozi na watendaji wa Mkoa wa Songwe na halmashauri ya Momba mkoani humo baada ya  hapo awali halmashauri ya Wilaya ya Momba kusuasua kutekeleza mradi wa ujenzi wa Maghalanmanne kupitia mradi Mkakati wa halmashauri mlipewa shilingi bilioni mbili.

Jafo alimwagiza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kukamilisha ujenzi wa maghala hayo lasivyo atolewe katika nafasi yake.

Leo hii katika ukaguzi wa mradi huo Waziri Jafo amekuta mradi huo  umetekelezwa vizuri sana kwa kujenga maghalanhayo manne yenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani elfu arobaini na nane.

Jafo amewapongeza watendaji wa halmashauri hiyo ya Momba na kuwataka waache tabia ya kufanyakazi kwa kusukumwa.

Aidha, Jafo alifanikiwa kukagua miradi mbalimbali Mkoani Songwe ikiwemo jengo la Ofisi ya Mkoa wa Songwe, Hospitali ya Mji wa Tunduma, pamoja na mradi wa Soko la Mazao la halmashauri ya Momba.
Share To:

Post A Comment: