NA HERI SHAABAN 

MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameagiza Wamiliki wa Shule binafsi kuruhusu wanafunzi wa shule za sekondari kufanya mitihani yao ya kidato cha sita ambayo inaanza Juni mwaka huu hata kama wanadaiwa hada.

Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema aliyasema hayo Wilayani Ilala leo Katika kikao cha kazi juu ya maelekezo kwa viongozi wa elimu ngazi ya wilaya na kata katika kipindi cha pili cha masomo baada ya likizo ya ugonjwa wa Karona .

"Katika wilaya yangu ya Ilala ufaulu kwa wanafunzi mzuri wilaya hii tumeshika nafasi ya tatu Kitaifa na mwaka huu tutafanya vizuri zaidi, hivyo naagiza     
watoto wote wasome na kufanya mitihani yao  ila wasipewe vyeti vyao mpaka wazazi wakilipa ada "alisema Mjema

Mjema aliwataka Wamiliki wa shule kuwabana wazazi wa wanafunzi wasizuie watoto kufanya mitihani  katika shule zao.

 Aidha Mjema aliwakumbusha Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt, John Magufuli inatekeleza sera ya elimu  bure kuanzia shule ya awali mpaka kidato cha nne lengo kuu la sera hiyo Ilani na maagizo ya viongozi wa Kitaifa ni kuakikisha watoto wote wa Tanzania wanapata elimu ya msingi bila kikwazo chochote hususani katika kufuta ada na michango yote ambayo ilionekana  kero na kikwazo kwa baadhi ya watoto wa kitanzania katika kupata elimu ya msingi  .

Akielezea hali ya ufaulu kwa mtihani wa Taifa Shule za Sekondari za halmashauri ya Ilala Mjema alisema hali ya ufaulu katika mitihani ya upimaji  kidato cha pili mwaka 2019 jumla ya wanafunzi 18,184 walifanya mtihani ukilinganisha na wanafunzi 16 ,792 waliofanya mtihani kwa mwaka 2018 kwa Miaka miwili mfululizo ufaulu asilimia 90 mwaka 2019 halmashauri ya ILALA ilikuwa ya 61 katika halmashauri 185.

Aidha alisema mwaka 2018 ilishika nafasi ya 63 matokeo hayo yalichangia mafanikio ya mkoa kushika nafasi ya 11 katika mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo kidato cha pili Ilala mwaka 2019 ilishika nafasi  tatu kwa asilimia 92 ya ufaulu  kwa halmashauri tano za mkoa Dar es salaam.

Akizungumzia kidato cha nne mwaka 2019 ufaulu ulikuwa asilimia 72.22 mwaka 2018 ufaulu asilimia 78  na kidato cha sita  mwaka 2019 ufaulu asilimia 98.19 mwaka 2018 walifaulu mtihani huo asilimia 96.32 .

Mwisho
Share To:

Post A Comment: