Msanii mkongwe katika industry ya muziki, "AY" anayetamba na kibao cha Danhela ala shavu la Ubalozi wa simu mpya ya Infinix NOTE 7.
Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, @infinixmobiletz waliweka viashiria vya ubalozi huo wiki iliyopita na siku ya Jumamosi, Mei 9 walithibitisha ubalozi huo kupitia LIVE Session ya Instagram iliyo onyesha wawakilishi wa Infinix wakifanya mazungumzo na AY kuhusiana na simu ya Infinix NOTE 7.
Infinix NOTE 7 imepewa jina la Bigi Makini, na ndio sababu kuu iliyopelekea Infinix kufanya kazi na AY, kwani wengi tunafahamu AY ni msanii mkongwe mwenye mafanikio makubwa mwenye kuheshimika kutokana na mchango wake katika game la muziki Tanzania.
Infinix NOTE 7 simu yenye umbo kubwa la inch 6.95 na speed ya ajabu ya G70 processor na kutokana na sifa hizi huenda Infinix NOTE 7 ndiyo simu yenye uwezo mkubwa na yenye kuvutia zaidi kwa mwaka huu wa 2020.
Ili kufahamu mengi zaidi kuhusiana na Infinix NOTE 7 na bidhaa nyengine za Infinix tafadhali tembelea kurasa zao za mitandao ya kijamii @infinixmobiletz
Kind regards Alex Mathias Sonna Chief Editor Fullshangwe Blog Email:alexsonna915@gmail.com Cellphone:+255653257072 Twitter:@ALEXSonna Instagram:@sonnaalex
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: