Thursday, 12 March 2020

WAZIRI WA NISHATI DK.KALEMANI ASEMA TRANSFOMA ZA KVA 11 ZIPO ZA KUTOSHA NCHINI...ATOA NENO

Na Mwandishi Wetu,Michuzi Blogu ya jamii

WAZIRI  wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amefanya ziara ya kikazi katika Kiwanda cha Tropical Industries kinachotengeneza nyaya na Transfoma kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa ziara zake kuona uwezo wa viwanda vya ndani katika uzalishaji wa vifaa muhimu vya umeme.

Akizungumza akiwa kiwandani hapo Dk.Kalemani amesema kuwa mahitaji ya ndani ya transfoma kwa mwaka ni 21,000  na kiwanda cha Tropical kina uwezo wa kuzalisha transfoma 75,000 kwa mwaka, hivyo hakuna sababu kwa TANESCO na Wakandarasi kuagiza vifaa hivyo kutoka nje ya nchi.

"Transfoma za kVA 11 ilikuwa ni kikwazo, baada ya kufika hapa nimejiridhisha zipo nyingi nawataka TANESCO na REA kuanzia kesho kupeleka vifaa hivyo maeneo yaliyokuwa na upungufu kama Singida, Tanga, Manyara na Kivule", amesema Dk.Kalemani. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tropical Charles Mlawa ameushukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John  Magufuli kwa kutoa vipaumbele kwa Watanzania kuwekeza katika Viwanda.

"Baada ya "Slogan" ya Mheshimiwa Rais kuwa Tanzania sasa ni nchi ya Viwanda, wao kama Watanzania walichukulia kauli mbiu yake kama fursa kwa kufungua kiwanda cha kutengeneza transfoma na waya

Mlawa ameongeza kiwanda hicho kinatengeneza waya za ABC na "high tension" lakini pia transfoma za kuanzia kVA 25 hadi kVA 5000.

Amesema mbali ya kupata tenda ndani ya nchi lakini pia nchi nyingine za Afrika kama Malawi na Kongo kupitia Lubumbashi.

Kiwanda cha Tropical Industries kinamilikiwa na Watanzania kwa asilimia 100 na Wafanyakazi wake wote ni vijana wa kitanzania. nj nchi ya Viwanda, sisi kama Watanzania tulichukulia slogani yake kama fursa kwa kufungua kiwanda cha kutengeneza transfoma na waya", amesema  Mlawa.

Ameongeza kiwanda hicho kinatengeneza waya za ABC na "high tension" lakini pia transfoma za kuanzia kVA 25 hadi kVA 5000.

Amesema mbali ya kupata tenda ndani ya nchi lakini pia nchi nyingine za Afrika kama Malawi na Kongo kupitia Lubumbashi.

Kiwanda cha Tropical Industries kinamilikiwa na Watanzania kwa asilimia 100 na Wafanyakazi wake wote ni vijana wa kitanzania.

No comments:

Post a comment