Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori(TAW) inatarajiwa kupokea Wawindaji wa kitalii 519 mwaka 2020 ambao wataingiza mapato kiasi cha shilingi bilioni 16.8

Naibu Kamishna wa TAWA, Iman Nkuwi alisema wawindaji wanaokuja nchini wameongezeka kutoka 434 wa mwaka 2018/19 Jana hadi kufikia 519 mwaka 2-19/20

Nkuwi amesema kipindi cha uwindaji wa kitalii hufanyika kuanzia mwezi julai hadi Desemba kila mwaka.

Amesema mapato hayo ya uwindaji kiasi cha sh 16.8 bilioni kitakacholipwa na wawindaji 519, hayajajumuisha fedha za malipo ya ada za vitalu vilivyopo nchini.
 
Mwaka uliopita tulipata kiasi cha sh 15.3 bilioni kutoka kwa wawindaji 434 hivyo ongezeko la mwaka huu linatokana na sababu ikiwepo maboresho yakanuni ambayo yameifanya Tanzania kuvutia wawindaji zaidi na kushindana na nchi nyingine za kusini mwa Afrika.

Kwa sasa Tanzania ina jumla ya vitalu vya uwindaji wa kitalii 88.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: