Monday, 16 March 2020

MSINGI WA UHALIFU WA KIMTANDAO UNATOKANA NA WENGI KUKURUPUKA KUTUMA TAARIFA BILA KUCHUNGUZA

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akifunga semina hiyo ya viongozi wa madhehebu ya dini kutoka Jumuiya ya maridhiano Kanda ya kaskazini iliyoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA jijini Arusha leo leo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Imeelezwa kukua kwa teknolojia ya mawasiliano nchini imepelekea uhalifu wa kimtandao kukua kwa kasi kutokana na teknolojia kutokuwa na mipaka na hivyo wahalifu kutumia mwanya huo kukamilisha adhma yao ya kiuhalifu.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo Cha Uhalifu wa Kimtandao kutoka Jeshi la Polisi nchini Joshua Mwangasa kwenye semina ya jinsi ya kujikinga na uhalifu katika huduma ya mawasiliano kwa viongozi wa madhehebu ya dini mkoa wa Arusha iliyoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA na kufanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Jijini hapa.

Alieleza kuwa bila ya kujua suala zima la kujikinga na masuala ya uhalifu wa kimtandao jamii itaendelea kutoa taarifa za uongo kufanya uhalifu huo hivyo semina hiyo imelenga kuwapa uelewa viongozi hao wa kiroho kuweza kuielimisha jamii kutoa taarifa zaidi za madhara ya kimtandao.

"Kutokujua sheria sio Kinga Wala kutekwa kifikra hivyo ni lazima uwe Makini sana na sms unazotumiwa uulize kwanza kwa muhusika hakikisha taarifa unayosambaza iwe sio ya uongo Wala yenye kudhalilisha jamii unapoweka taarifa zako kwenye mtandao Toa taarifa sahihi ikiwemo taarifa za kiuhalifu"

Kwa upande waka Mratibu wa Semina hiyo Mabel Masasi ambaye pia ni Afisa mahusiano wa TCRA alisema kuwa sheria za kimtandao zinatakiwa jamii kuzijua ili kuondoa changamoto ya makosa ya kimtandao kwani wengi wanatumia mitandao ya kijamii kwa mambo yasiofaa na hayana maslahi na maendeleo yao na taifa.

Alisema kuwa semina hiyo itaendeshwa nchi nzima na hadi Sasa mikoa minne teyari wameshapata mafunzo hayo ikiwemo Arusha na mkoa unaofuata ni Dodoma hivyo ni muhimu kwetu kuangalia na kutoa taarifa za makosa ya kimtandao Polisi.

"Niwasihi Sana ndugu zangu viongozi wa kiroho kutoa elimu kwa jamii kujua huduma za mawasiliano ya mitandao ili kuondoa wimbi la mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii inayotokana na matumizi yasio sahihi ya mitandao ya kijamii ikiwemo wale wanaotuma taarifa zisizo sahihi hivyo elimu ndio msingi wa kuondoa changamoto"

Alisema Kuna vitu vinatakiwa kuzingatia wakati unanunua simu au laini ya simu kwani inawezekana kuwa umeingia kwenye mkataba bila kujua hivyo ni wajibu kusoma maelekezo ili usije kuingia kwenye vigezo na masharti kuzingatiwa bila kujua tuwe Makini sana

Awali Wenyeviti wenza wa kamati ya maridhiano Mkoa wa Arusha wameishukuru Sana TCRA kuweza kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatasaidia kuweza kuondoa changamoto ya uvunjifu maadili kwenye jamii yetu hususani makosa ya kiuhalifu kwa njia ya kimtandao.

Sheikh wa wilaya Husein Ijunju alisema kuwa semina hiyo imewafungua na kupata uelewa mpana wa makosa ya Kimtandao hivyo watatoa ushirikiano kusaidia jamii wanayoiongoza kuweza kutumia mtandao kwa njia zilizo kubalika badala ya kutumia kwa njia zinazovunja maadili au kutuma maudhui yasiokubalika yanaoharibu maadili yetu.

Akaitaka mamlaka hiyo kuongeza wigo wa utoaji elimu na muda wa mafunzo hayo kuongezwa ili kupata uelewa mpana wa mafunzo hayo ambayo wanaona yatasaidia kuondoa changamoto ya matumizi yasio sahihi ya mitandao ya kijamii. 

Nae Askofu Jacob Mwaigagu alisema kuwa wananchi wamekuwa na hofu kubwa ya kutoa taarifa fiche za kiuhalifu kwa Jeshi la Polisi wakihofia taarifa hizo kuweza kumfikia mhalifu kuwa aliye toa taarifa hii mtu fulani jambo linalohatarisha watu wengi kwani Siri nyingi zimekuwazikivuja.
No comments:

Post a comment