Saturday, 14 March 2020

MCHUNGAJI MALEKANA:TUTATUMIA MAKONGAMANO ,IBAADA NA VYOMBO VYA HABARI VYA KANISA KUELIMISHA WAUMINI KUPINGA UNYANYAPAA KWA WENYE VVUNa.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Askofu mkuu wa jimbo la Kusini Mwa Tanzania Kanisa la Waadventista
Wasabato  Tanzania Mch.Mark Walwa Malekana amesema kwa niaba ya Kanisa
la Waadventista Wasabato Tanzania ,kanisa litatumia makongamano
mbalimbali ya vijana,wanawake,na ibaada pamoja na vyombo mbalimbali
vya kanisa katika kuelimisha jamii juu ya kutokomeza unyanyapaa.

Mchungaji Malekana aliyasema hayo jijini Dodoma katika uzinduzi wa
 kampeni ya kushirikisha viongozi wa dini kwa   kupinga unyanyapaa kwa
waishio na Virusi vya UKIMWI pamoja  ukatili dhidi ya wanawake na
watoto  inayokwenda kwa kauli mbiu isemayo “Hebu Tuyajenge tufikie
95-95-95 ,tuungane  kutokomeza  dhidi ya unyanyapaa  wa VVU na UKIMWI
Tanzania.“Sisi kama viongozi wa dini tunataendelea kuelimisha waumini pamoja na jamii kwa ujumla kupitia makongamano ya vijana,makambi,na ibaada za kanisani pamoja na vyombo vyetu vya kanisa kuhakikisha elimu ya kupinga unyanyapaa kwa waishio na Virusi vya UKIMWI pamoja na kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto”alisema.
Spika wa bunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai
alisema bado kuna unyanyapaa  wa kupima VVU huku Mkurugenzi mtendaji
wa baraza la waishio na VVU nchini ,NACOPHA,Deogratius Rutatwa akisema
 ni vyema kukaa pamoja na kuyajenga na kushikamana katika kutokomezaWaziri mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hiyo alisema   lengo la kongamano hilo ni kusisitiza upendo na
kuwathamini wenye matatizo na kuwatia faraja hivyo viongozi wa dini
wana nafasi kubwa katika kuelimisha waumini wao katika kuelimisha juu
ya madhara ya unyanyapaa katika jamii.

Aidha,Waziri Mkuu Majaliwa alisema  kuanzia sasa ni marufuku kwa mtu yeyote
kutamka neno”waathirika  wa UKIMWI “Kwani lina unyanyapaa na badala
yake kutumia neno”Wenye maambukizi ya UKIMWI.

Mwakilishi kutoka serikali ya watu wa Marekani[USAID]Gray Saga alisema
vifo vitokanavyo na maambukizi mapya ya VVU vimepungua kwa asilimia
80%    na hivyo Serikali ya Marekani  imedhamiria kuendelea kuisaidia
Tanzania kwa kushirikiana na viongozi wa dini katika mapambano dhidi
ya VVU na UKIMWI ambapo imewekeza zaidi ya dola za Kimarekani Bilioni
4.8  kwa miaka 15 iliyopita.

No comments:

Post a comment