Mtuhumiwa wa mauaji ya mfanyakazi wa ndani Salome Zakaria 19 Mkami Shirima akiingizwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi Arumeru chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polisi picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Mtuhumiwa Mkami Shirima picha yenye kuzungushiwa akiyeinamisha kichwa akiingia makahamani kujibu tuhuma za mauaji ya Marehemu  Salome Zakaria

Wananchi wakiwa wanafuatlia kumjua mtuhumiwa Mkami Shirima wa mauaji ya binti wa kazi Marehemu Salome Zakaria 

Mkami Zakaria mtuhumiwa wa mauaji ya binti wa kazi eneo la Elkuirei wilayani Arumeru akiingizwa mahakamani chini ya Askari kanzu wa kike kwenye mahakama ya hakimu mfawidhi wilaya hiyo leo


Gari iliyombeba mtuhumiwa wa mauaji ikitoka nje ya mahakama ya hakimu mfawidhi wilaya ya Arumeru picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha
Arusha
Taharuki imetanda kwenye mahakama ya hakimu mkazi Arumeru wakati mtuhumiwa wa mauaji ya binti wa kazi Mkami Shirima baada ya kufikishwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi wenye silaha kali na mabomu ya machozi.

Mara baada ya kufikishwa mahakamani hapo akiwa kwenye gari binafsi aina ya Nadia chini ya Askari wa kike na wakiume  wenye silaha kali ndipo alipandishwa kwenye kizimba majira ya saa sita mchana na kusomewa mashtaka ya mauaji mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Arumeru Analia Mushi .

Kesi hiyo namba tano ya mwaka 2020 aliyosemewa mshtakiwa huyo ambaye hakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo itarudi kutajwa Tena tarehe 26 mwezi huu na mshatakiwa kupelekwa gereza la Kisongo akiwa kwenye gari aina ya Raum.

Ilielezwa mahakamani hapo kwamba mnamo tarehe sita mwezi wa tatu huu huko maeneo ya mianzini mtuhimiwa Mkami Shirima alimpiga mfanyakazi wake Salome Zakaria ambaye ni marehemu kwa Sasa akijua ni kosa kisheria.

Katika hali isiyo ya kawaida Polisi waliotanda mahakamani hapo waliwazuia waandishi wa habari kufanya majukumu yao baada ya kuzuia kuingia kwenye chumba Cha mahakama kusikiliza kesi hiyo huku wakimkinga mtuhumiwa wasimpige picha za matukio jambo lililozua taharuki mahakamani hapo kwa muda.

Hata hivyo mtuhumiwa Shirima alipotoka mahakamani hapo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi wakiongozwa na OCCID ambaye aliwazuia wanahabari kutenda majukumu yao ikiwemo kupata picha za matukio ya mtuhumiwa huyo.

Jambo hilo limeibua sintofahamu ambayo inaonyesha Polisi hao kumlinda mtuhumiwa ambaye ni mke wa Askari Mwenzao na kuleta hisia tofauti kwa waandishi wa habari kuzungushwa kupata kibali Cha kuandika habari hiyo.

Hata hivyo mtuhumiwa Shirima alisafirishwa na Gari binafsi aina ya Raum lenye no za usajili T497 DEM lenye tinted nyeusi kuelekea gereza la Kisongo chini ya ulinzi wa gari mbili za Jeshi la Polisi.

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: